RUNGU LA TFF HALIJAMWACHA CHIRWA SALAMA - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Friday, 5 January 2018

RUNGU LA TFF HALIJAMWACHA CHIRWA SALAMA


Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi (Saa 72) iliyokutana jana Januari 4, 2018 imejadili mechi mbalimbali za Ligi Kuu (VPL) Daraja la Kwanza (FDL) na Daraja la Pili (SDL).

LIGI KUU YA VODACOM


Mechi namba 72 (Mbeya City 0 vs Simba 1).Kamishna wa mechi hiyo Billy Mwilima amepewa Onyo Kali kwa kuruhusu mchezaji Hamisi Msabila wa Mbeya City kucheza mechi bila kuonyesha leseni, hivyo kukiuka Kanuni ya 14(16 na 17) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.
Mechi namba 81 (Ndanda 1 vs Njombe Mji 1). Klabu ya Ndanda imepigwa faini ya sh 500,000 (laki tano) kwa kutowasilisha orodha ya wachezaji wake (team match list) kwenye kikao cha maandalizi ya mechi (pre- match meeting) kama ilivyoainishwa katika Kanuni ya 14(2k) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo. Adhabu dhidi ya Ndanda katika mechi hiyo iliyofanyika Novemba 24, 2017 kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 14(3) ya Ligi Kuu.
Pia Kamati imeiomba Sekretarieti ya Bodi ya Ligi kutoa Waraka mwingine kwa klabu kuzikumbusha kuhusu kutoa orodha ya wachezaji kwenye kikao cha maandalizi ya mechi (pre-match meeting).
Mechi namba 83 (Yanga 1 vs Tanzania Prisons 1). Tanzania Prisons imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) baada ya kuhudhuria kikao cha maandalizi ya mechi (pre-match meeting) ikiwa na maofisa watatu badala ya wanne, hivyo kwenda kinyume na Kanuni ya 14(2b) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.
Adhabu dhidi ya Tanzania Prisons katika mechi hiyo iliyochezwa Novemba 25, 2017 Uwanja wa Azam Complex ni kwa mujibu wa Kanuni ya 14(3) ya Ligi Kuu.
Wachezaji Lambart Sabiyanka wa Tanzania Prisons na Obrey Chirwa wa Yanga wamesimamishwa kwa kuzingatia Kanuni ya 9(5) ya Ligi Kuu kutokana na kufanya vitendo vya utovu wa nidhamu, wakisubiri malalamiko dhidi yao kusikilizwa na Kamati ya Nidhamu ya TFF.
Pia Kamati imeiomba TFF iipatie Bodi ya Ligi uamuzi (ruling) wa Kamati ya Nidhamu juu ya mchezaji wa Yanga kusimamishwa baada ya mechi dhidi ya Mbao FC wakati akisubiri mashtaka yake ili kuufanyia kazi kwa ajili ya mapendekezo ya marekebisho ya Kanuni.
Mechi namba 84 (Mbao 1 vs Mwadui 0). Klabu ya Mbao FC imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kutokana na washabiki wake kuruka uzio wa ndani na kwenda kushangilia katika eneo lisiloruhusiwa katika mechi iliyochezwa Novemba 25, 2017 Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.


Adhabu dhidi ya Mbao FC ni uzingativu wa Kanuni ya 42(1) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Klabu.


Mechi namba 90 (Lipuli 0 vs Tanzania Prisons 1).Mtunza Vifaa wa Lipuli FC, George Mketo amesimamishwa akisubiri suala lake la kuwatukana waamuzi katika mechi hiyo iliyofanyika Desemba 30, 2017 Uwanja wa Samora mjini Iringa kusikilizwa na Kamati ya Nidhamu. Uamuzi wa kumsimamisha umezingatia Kanuni ya 9(5) ya Ligi Kuu kuhusu Usimamizi wa Ligi.EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati http://www.edusportstz.com ni fahari ya wasomaji
UNGANA NASI KUPITIA LIKI HIZI ILI KUTUMIWA HABARI POPOTE ULIPO

EDUSPORTSTZ NI FAHARI YA WASOMAJI

WEKA EMAIL YAKO:


Delivered by EDUSPOTSTZ
Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno
EDUSPORTSTZ