KWA REKODI HII, YANGA YAANZA KUNUSIA HATUA YA NUSU FAINALI MAPINDUZI CUP - EDUSPORTSTZ

Latest

KWA REKODI HII, YANGA YAANZA KUNUSIA HATUA YA NUSU FAINALI MAPINDUZI CUP

Image result for YANGA SC



Wachezaji wa timu ya Yanga SC.

MLINZI wa kulia wa Yanga, Hassan Kessy jana Alhamisi alikuwa shujaa wa timu yake baada ya kufunga bao pekee katika ushindi wa bao 1-0 dhidi ya JKU katika mchezo wa hatua ya makundi ya michuano ya Kombe la Mapinduzi inayoendelea visiwani Zanzibar.

Kessy aliwaduwaza wata­zamaji wengi wa mechi hiyo waliodhani mechi hiyo ita­malizika kwa suluhu, lakini alifanikiwa kufunga bao hilo dakika ya 90.

Huo ni ushindi wa pili kwa Yanga katika michuano hiyo ambapo awali ilicheza dhidi ya Mlandege na kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Kwa ushindi huo wa jana, Yanga hivi sasa inashika nafasi ya pili katika Kundi B nyuma ya Singida United inayoongoza kundi hilo. Timu hizo zote zina pointi sita sawa na Mlandege, lakini zinatofautiana mabao ya kufunga na kufungwa.

Yanga ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara kwa ushindi huo wamefanikiwa kuvunja mwiko wa kuifunga JKU baada ya kupita mechi mbili mfululizo ambazo zote waliambulia kichapo, mchezo mmoja wa Mapinduzi misimu miwili iliyopita walifungwa bao 1-0 na Amour Janja na ule wa kirafiki uliofanyika katika Uwanja wa Uhuru, Dar am­bao walifungwa mabao 2-0.

Katika hatua nyingine jana mchana uwanjani hapo Singida United walimalizia mechi yao kiporo dhidi ya Taifa Jang’ombe ambayo ilishindwa kumalizika juzi Juma­tano baada ya mvua kubwa na kuufanya mchezo huo kuvun­jika. Mpaka mchezo huo unavunjika, Singida ilikuwa inaongoza mabao 3-1.

Kutokana na ushindi huo Yanga ina nafasi kubwa ya kusonga mbele na kufuzu hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo, ambapo imesaliwa na michezo miwili kukamilisha hatua ya makundi.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati http://www.edusportstz.com ni fahari ya wasomaji
UNGANA NASI KUPITIA LIKI HIZI ILI KUTUMIWA HABARI POPOTE ULIPO

EDUSPORTSTZ NI FAHARI YA WASOMAJI

WEKA EMAIL YAKO:


Delivered by EDUSPOTSTZ
Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno
EDUSPORTSTZ


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz