PACHA HATARI ZAIDI YA WACHEZAJI LIGI KUU TANZANIA VPL MSIMU HUU - EDUSPORTSTZ

Latest

PACHA HATARI ZAIDI YA WACHEZAJI LIGI KUU TANZANIA VPL MSIMU HUU



Hadi raundi ya kwanza ya ligi kuu Tanzania bara inamalizika, Emanuel Okwi na John Bocco ndio pacha hatari zaidi.
Kwa pamoja Okwi na Bocco wamefunga magoli 19 kwenye ligi, Okwi akifunga magoli 12 huku Bocco yeye akiwa amefunga magoli saba (7).

Leo Januari 28, 2018 wawili hao kwa pamoja wamefunga magoli manne dhidi ya Majimaji FC katika mchezo wa ligi uliochezwa uwanja wa taifa.



Bocco alianza kufunga goli la kwanza kwa kichwa baada ya kutokea piga-nikupige kwenye goli la Majimaji, mshambuliaji huyo aliyesajiliwa kutoka Azam akafunga pia goli la pili huku Okwi akifunga bao la tatu na la nne.

Simba wamefikisha pointi 35 na kuendelea kuongoza kwenye msimamo wa ligi baada ya kukamilisha mechi 15 za mzunguko wa kwanza. Simba imeendeleza gape la pointi dhidi ya wapinzani wake kwenye mbio za ubingwa wa VPL, iko mbele kwa pointi tano dhidi ya Azam, pointi saba mbele ya Yanga huku Singida United na Mtibwa ziachwa kwa pointi nane na tisa.


Simba imefunga magoli mengi zaidi ya timu yoyote katika mechi tatu za mwisho za mzunguko wa kwanza , imefunga jumla ya magoli 10 katika mechi tatu zilizopita huku yenyewe ikiwa haijaruhusu goli katika mechi hizo (Simba 4-0 Singida United, Kagera Sugar 0-2 Simba, Simba 4-0 Majimaji).


Kocha mpya wa simba Pierre Lechantre ameiongoza timu hiyo kwa mara ya kwanza na kupata ushindi mzuri kwenye mchezo wake wa kwanza akiongoza benchi la ufundi la klabu hiyo tangu aliposaini mkataba kuitumikia Simba Januari 19, 2018.


Simba inaendelea kubaki kuwa klabu pekee ambayo haijapoteza mchezo hadi sasa baada ya kumaliza mzunguko wa kwanza (mechi 15) hiyo ni baada ya Yanga kuivunja rekodi ya Azam ya kutopoteza mchezo wa ligi kwa kuifunga 2-1 kwenye uwanja wa Azam Complex.NDG MSOMAJI WA EDUSPORTSTZ UNAKUMBUSHWA KUSUBSCRIBE NA KUFOLLOW WEB YETU PAMOJA NA MITANDAO YETU YA KIJAMII CHINI YA POSITI HII ILI KUTUMIWA UPDATES ZOTE ZA AJIRA, MICHEZO, HABARI, SCHOLARSHIPS PAMOJA NA MASTORI YA MASTAA NA VIONGOZI MBALIMBALI. EDUSPOTSTZ NI FAHARI YA WASOMAJI.
EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati. BOFYA HAPA KUJIUNGA NA INNOVATION FURSA CHALLENGE http://www.edusportstz.com ni fahari ya wasomaji
UNGANA NASI KUPITIA LIKI HIZI ILI KUTUMIWA HABARI POPOTE ULIPO

EDUSPORTSTZ NI FAHARI YA WASOMAJI

WEKA EMAIL YAKO:


Delivered by EDUSPOTSTZ
Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno
EDUSPORTSTZ


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz