OXLADE-CHAMBERLAIN:KUONDOKA KWA COUTINHO HAKUTAATHIRI LIVERPOOL - EDUSPORTSTZ

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Friday, 12 January 2018

OXLADE-CHAMBERLAIN:KUONDOKA KWA COUTINHO HAKUTAATHIRI LIVERPOOL


Coutinho na Oxlade-Chamberlain

Kuondoka kwa Philippe Coutinho hakutaathiri klabu ya Liverpool kivyovyote kulingana na kiungo wa kati wa klabu hiyo Alex Oxlade-Chamberlain.

Coutinho, ambaye alifunga mabao 54 katika mechi 201 akiichezea Liverpool, aliondoka Anfield akielekea Barcelona kwa dau la £142m wiki iliopita.

"Wakati Phil alipowekwa benchi tulikuwa tukicheza mchezo mzuri na bado tuna wachezaji wazuri ambao wanaweza kufunga mabao ', alisema Oxlade-Chamberlain.

"Nina imani na vijana wenzangu kwamba tuendelee tulivyo .Sidhani kama itatuathiri kivyovyote''.

Mchezaji huyo wa Uingereza aliongezea: Sijawahi hata kufikiria kwamba Phil ameondoka.

"Wakati mchezaji wa haiba yake anapoondoka , ameondoka. Upo katika klabu kama Liverpool na mchezaji mwengine mkubwa atajitokeza katika siku za usoni."

Oxlade-Chamberlain, ambaye ameanzishwa katika mechi saba za ligi ya Uingereza tangu uhamisho wake kutoka Arsenal huenda akapewa fursa zaidi baada ya Coutiunho kuondoka..

"kwa kweli ni fursa kwangu mimi ,kama ilivyo kwa wachezaji wengine wote'' , alisema.

No comments:

Post a Comment