NEYMAR AZOMEWA KISA HIKI HAPA - EDUSPORTSTZ

Latest

NEYMAR AZOMEWA KISA HIKI HAPA


NDG MSOMAJI WA EDUSPORTSTZ UNAKUMBUSHWA KUSUBSCRIBE NA KUFOLLOW WEB YETU PAMOJA NA MITANDAO YETU YA KIJAMII CHINI YA POSITI HII ILI KUTUMIWA UPDATES ZOTE ZA AJIRA, MICHEZO, HABARI, SCHOLARSHIPS PAMOJA NA MASTORI YA MASTAA NA VIONGOZI MBALIMBALI. EDUSPOTSTZ NI FAHARI YA WASOMAJI.

Neymar alizomwa na mashabiki wa Paris St-Germain baada ya kumnyima Edinson Cavani fursa ya kuwa mchezaji aliyeifungia klabu hiyo mabao mengi wakati wa mechi dhidi ya Dijon

Neymar alizomewa na mashabiki wa Paris St-Germain baada ya kumnyima Edinson Cavani fursa ya kuwa mchezaji aliyeifungia klabu hiyo mabao mengi wakati wa mechi dhidi ya Dijon.

Bao la kipindi cha kwanza la Cavani lilimfanya kuwa sawa kwa magoli na mshambuliaji wa zamani Zlatan Ibrahimovic akiwa na magoli 156 katika mashindano yote aliyochezea PSG.

Wenyeji hao waliongoza kwa 4-0 katika kipindi cha kwanza na Neymar alikuwa tayari amekamilisha hat-trick kabla ya PSG kupata penalti.

Hatahivyo raia huyo wa Brazil aliamua kupiga mkwaju huo wa penalti badala ya kumwachia Cavani, hatua iliomfanya Neymar kuzomwa na mashabiki wa timu hiyo , lakini kocha Unai Emery alimtetea mchezaji huyo baada ya mechi hiyo.Image captionNeymar na Cavani wakishindana ni nani anayefaa kupiga penalti

''Nadhani Neymar alipiga mkwaju huo wa penalti kwa sababu ilikuwa siku nzuri kwake'', alisema Emery.

''Tunafurahia. Lakini kutakuwa na fursa nyingi kwa Cavani kufunga mabao zaidi''.

Beki wa PSG Thomas Meunier aliitaja hatua hiyo ya Neymar kuwa aibu lakini akaongezea kuwa ni Neymar aliyepewa jukumu la kupiga penalti.

''Angempatia mpira ingekuwa ishara nzuri ya fair Play'', alisema.

''Aliifanyia kazi kubwa timu yetu na swala la kuzomwa na mashabiki , kwa kweli hakuipiga vizuri. Nadhani wachezaji wengi wangefanyiwa hivyo''.Haki miliki ya pichaTWITTERImage captionMshambuliaji wa PSG Edinson Cavani

PSG inaongoza kwa pointi 11 kutoka kwa wapinzani wake wa karibu Lyon baada ya mechi 21.

Vionghozi hao wa ligi wameshinda mechi nane zilizopita na michuano ya kuwania mataji, wakiwa wamefunga mabao 31 na kufungwa sita pekee.

Dijon ambao wako katika nafasi ya 11 katika jedwali hawajashinda hata mechi moja katika mechi nne walizocheza.NDG MSOMAJI WA EDUSPORTSTZ UNAKUMBUSHWA KUSUBSCRIBE NA KUFOLLOW WEB YETU PAMOJA NA MITANDAO YETU YA KIJAMII CHINI YA POSITI HII ILI KUTUMIWA UPDATES ZOTE ZA AJIRA, MICHEZO, HABARI, SCHOLARSHIPS PAMOJA NA MASTORI YA MASTAA NA VIONGOZI MBALIMBALI. EDUSPOTSTZ NI FAHARI YA WASOMAJI.
EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati. BOFYA HAPA KUJIUNGA NA INNOVATION FURSA CHALLENGE http://www.edusportstz.com ni fahari ya wasomaji
UNGANA NASI KUPITIA LIKI HIZI ILI KUTUMIWA HABARI POPOTE ULIPO

EDUSPORTSTZ NI FAHARI YA WASOMAJI

WEKA EMAIL YAKO:


Delivered by EDUSPOTSTZ
Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno
EDUSPORTSTZ


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz