ARSENAL WENGER ADAIWA KUIKOSEA HESHIMA DORTMUND KUHUSU AUBAMEYANG - EDUSPORTSTZ

Latest

ARSENAL WENGER ADAIWA KUIKOSEA HESHIMA DORTMUND KUHUSU AUBAMEYANG





NDG MSOMAJI WA EDUSPORTSTZ UNAKUMBUSHWA KUSUBSCRIBE NA KUFOLLOW WEB YETU PAMOJA NA MITANDAO YETU YA KIJAMII CHINI YA POSITI HII ILI KUTUMIWA UPDATES ZOTE ZA AJIRA, MICHEZO, HABARI, SCHOLARSHIPS PAMOJA NA MASTORI YA MASTAA NA VIONGOZI MBALIMBALI. EDUSPOTSTZ NI FAHARI YA WASOMAJI.

Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger ''alitukosea heshima'' kwa kuzungumza hadharani kuhusu mchezaji Pierre-Emerick Aubameyang, amesema mkurugenzi wa michezo katika klabu ya Borussia Dortmund Michael Zorc.

Arsenal ina hamu ya kumsajili mshambuliaji huyo wa Gabon kwa dau la £60m.

Siku ya Alhamisi , Wenger alisema kuwa Aubameyang atafaa sana Arsenal , matamshi ambayo hayakuifurahisha klabu ya Dortmund.

''Tunahisi kwamba ni kukosa heshima kwa Wenger kuzungumzia kuhusu wachezaji wa klabu nyengine'', alisema Zorc.

''Hatujawasiliana na Arsenal''.

''Kwa sasa Arsene Wenger ana maswala mengi yanayompa changamoto ikiwemo mchezo wa wachezaji wake''.

Aubameyang ameadhibiwa mara mbili kwa utovu wa nidhamu msimu huu.Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger

Alikosa mechi ya Jumapili ya sare ya 0-0 dhidi ya Wolfsburg baada ya kukosa kuhudhuria mkutano wa timu.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 ni mfungaji wa mabao mengi katika timu hiyo msimu huu baada ya kufunga mabao 13 katika mechi 15.

Dortmund ni ya nne katika ligi ya Bundesliga, wakiwa na alama 15 nyuma ya viongozi wa ligi Bayern Munich
EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati. BOFYA HAPA KUJIUNGA NA INNOVATION FURSA CHALLENGE http://www.edusportstz.com ni fahari ya wasomaji
UNGANA NASI KUPITIA LIKI HIZI ILI KUTUMIWA HABARI POPOTE ULIPO

EDUSPORTSTZ NI FAHARI YA WASOMAJI

WEKA EMAIL YAKO:


Delivered by EDUSPOTSTZ
Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno
EDUSPORTSTZ


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz