MESSI HUENDA AKAONDOKA BARCELONA BUREE - EDUSPORTSTZ | Habari za Ajira, Mapenzi, Michezo, Elimu, Kilimo, Technology, Siasa na Mziki,

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Friday, 5 January 2018

MESSI HUENDA AKAONDOKA BARCELONA BUREE
Hii inaweza kuwa bahati ya mtende kwa vilabu vingine vya soka barani Ulaya, kuna hatari kwamba mwanasoka anayetajwa kwamba bora kuwahi kutokea duniani Lioneil Messi anaweza akaondoka bure Barcelona.

Hii inaweza kutokea kama jimbo la Catalunya nchini humo litapata uhuru wake, Catalunya ndio mji wanaotokea Barcelona na kwa muda sasa wamekuwa wakidai uhuru wao kutoka kwa taifa la Hispania.

Mara kadhaa serikali ya Hispania imekuwa ikizuia jaribio la Wacatalunya kuwa nchi huru na mwaka jana nguvu kubwa ilitumika kuzima jaribio kubwa la raia wa Catalunya kudai uhuru wao kutoka Hispania.

Bado Catalunya hawajakata tamaa kuhusu suala la uhuru wao na endapo hilo litafanikiwa baasi Barcelona watatolewa katika michuano ya La Liga ambayo iko katika taifa la Hispania na kutafuta ligi yao.

Haijafahamika wazi kwamba ni wapi Barcelona wataelekea na haifahamiki kwamba watakuwepo kwenye orodha ya UEFA, na Messi inafahamika hataweza kukaa katika klabu ambayo haitakuwa ikishiriki ligi kubwa.

Gazeti moja la michezo nchini Hispania linasema katika kipengele cha mkataba wa Lioneil Messi kipo kipengele ambacho kinamfanya mchezaji huyo kuachana na Barcelona endapo hawatakuwa katika michuano mikubwa.

Manchester City, Chelsea na PSG mara kadhaa wametajwa kummezea mate mchawi huyu wa soka na kama hili likitokea huenda ikawa nafasi yao kushindana kumshawishi Lioneil kujiunga na timu hizo
EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati http://www.edusportstz.com ni fahari ya wasomaji
UNGANA NASI KUPITIA LIKI HIZI ILI KUTUMIWA HABARI POPOTE ULIPO

EDUSPORTSTZ NI FAHARI YA WASOMAJI

WEKA EMAIL YAKO:


Delivered by EDUSPOTSTZ
Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno
EDUSPORTSTZ

No comments:

Post a Comment