LIGI DARAJA LA KWANZA YAJA NA MVUTO USIO KIFANI - EDUSPORTSTZ

Latest

LIGI DARAJA LA KWANZA YAJA NA MVUTO USIO KIFANI



NDG MSOMAJI WA EDUSPORTSTZ UNAKUMBUSHWA KUSUBSCRIBE NA KUFOLLOW WEB YETU PAMOJA NA MITANDAO YETU YA KIJAMII CHINI YA POSITI HII ILI KUTUMIWA UPDATES ZOTE ZA AJIRA, MICHEZO, HABARI, SCHOLARSHIPS PAMOJA NA MASTORI YA MASTAA NA VIONGOZI MBALIMBALI. EDUSPOTSTZ NI FAHARI YA WASOMAJI.

Jana kulikuwa  na mechi za hatari ligi daraja la kwanza ikiwa ni mechi za mwishomwisho ambazo zinaamua timu za kupanda daraja kucheza ligi kuu tanzania bara msimu ujao 2018/19.

Mambo yalinoga kwenye mchi za Kundi C ambapo zitachezwa mechi nne, mechi tatu kazi ya hizo zikishirikisha timu tatu (Biashara United, Dodoma FC na Alliance Schools) ambazo zilipambana kutafuta nafasi mbili za kupanda daraja kucheza VPL msimu ujao.

Mechi za Kudi C zilizo chezwa jana
JKT Oljoro vs Dodoma FC
Pamba SC Toto Africans
Biashara United vs Rhino Rangers
Transist Camp vs Alliance Schools

Kundi B ulichezwa mchezo mmoja
Mawenzi Market vs Mbeya Kwanza

Kocha wa Dodoma FC Jamhuri Kihwelu ‘Julio’ alisema haitapendeza uwanja wa kisasa ujengwe dodoma halafu kusiwe na timu inayocheza ligi kuu.

“Tunajua ligi daraja la kwanza ngumu, hakuna anaetaka kupoteza kizembe, kwa hiyo nataka niseme tunafahamu mechi itakuwa ngumu lakini kwa sababu tuna dhamira ya makusudi ya kutaka kupanda ligi kuuu huku ukichukulia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amesema uwanja wa kisasa ujengwe Dodoma sasa inakosekana vipi timu ya ligi kuu.”

“Tunatakiwa tujitoe kuhakikisha kwamba tunapata nafasi hiyo, tunajua Oljoro ni moja ya timu nzuri lakini bahati mbaya ponti zao sio nyingi wala hazitasaidia kufanya lolote hata kama watashinda mechi zote zilizosalia hawana nafasi ya kupanda wala hawashuki daraja. Timu akama hizo zinacheza zikiwa hazina presha tofauti na sisi ambao tuna tension kwa sababu kuna kitu tunatafuta.”

Kundi C linaongozwa na Biashara United ikiwa na pointi 23 ikifuatiwa na Dodoma FC yenye pointi 21 wakati Alliance Schools wao wakiwa na pointi 19 kwenye msaimamo, mechi za leo huenda zikabadili msimamo wa kundi hilo.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati. BOFYA HAPA KUJIUNGA NA INNOVATION FURSA CHALLENGE http://www.edusportstz.com ni fahari ya wasomaji
UNGANA NASI KUPITIA LIKI HIZI ILI KUTUMIWA HABARI POPOTE ULIPO

EDUSPORTSTZ NI FAHARI YA WASOMAJI

WEKA EMAIL YAKO:


Delivered by EDUSPOTSTZ
Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno
EDUSPORTSTZ


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz