KUNG'OLEWA KWA SIMBA MAPINDUZI CUP MASHABIKI WAANZA KUSHIKANA UCHAWI - EDUSPORTSTZ

Latest

KUNG'OLEWA KWA SIMBA MAPINDUZI CUP MASHABIKI WAANZA KUSHIKANA UCHAWI


Kung’olewa kwa Simba katika michuano ya Kombe la Mapunduzi baada ya kuchapwa bao 1-0, kumezua mjadala mpya kuhusiana na Kocha Joseph Omog.



SIMBA MANUSULA WAPOTEZE MCHEZO WAO DHIDI YA MTIBWA SUKARI


Omog raia wa Cameroon, alifungashiwa virago vyake na uongozi wa Simba ambao ulitumia maneno matamu kusema wamekubaliana aondoke baada ya kuvuliwa ubingwa wa Kombe la Shirikisho na Green Worries inayoshiriki ligi daraja la pili.

Lakini baada ya kipigo cha leo, mashabiki wameanza kuhoji kama ilikuwa sahihi kumuondoa Omog.

Baadhi ya mashabiki wa Simba na wa timu nyingine wameeleza kuwa Simba ilikurupuka kumuondoa kocha huyo.

Lakini wako waliosema tatizo kubwa ni wachezaji wenyewe ambao wameshindwa kujituma na kuonyesha wanataka kushinda.


Pia kuna mashabiki ambao wameelekeza lawama zao moja kwa moja kwa Kocha Irambona Masoud Djuma kwamba mfumo wake unaonekana kuwa mgumu na si imara katika ulinzi.


Kipigo hicho leo kwenye Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar kimekuwa cha pili mfululizo kwa Simba.


Mechi iliyopita, Simba ilikutana na kipigo kama hicho kutoka kwa Azam FC na matumaini yao kuendelea ilikuwa leo dhidi ya URA.



Bao la URA lilipatikana dakika za nyongeza za kipindi cha kwanza na kipindi chote cha pili, Simba ilishindwa kupata angalau bao moja.


EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati. BOFYA HAPA KUJIUNGA NA INNOVATION FURSA CHALLENGE http://www.edusportstz.com ni fahari ya wasomaji
UNGANA NASI KUPITIA LIKI HIZI ILI KUTUMIWA HABARI POPOTE ULIPO


EDUSPORTSTZ NI FAHARI YA WASOMAJI

WEKA EMAIL YAKO:


Delivered by EDUSPOTSTZ
Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno
EDUSPORTSTZ


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz