KARIA ATOA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KIFO CHA CHAMA - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

DOWNLOAD AJIRA DAILY HAPA

Monday, 8 January 2018

KARIA ATOA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KIFO CHA CHAMARais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars”
Athuman Juma “Chama” maarufu kama Jogoo aliyefariki usiku wa kuamkia leo Januari 8, 2018 kwenye hospitali ya Taifa Muhimbili.


Katika salamu hizo za rambirambi Rais Karia amesema ni mshtuko mkubwa kumpoteza mchezaji huyo wa zamani na ametoa pole kwa familia yake,ndugu jamaa na marafiki.


Rais Karia amesema TFF inatoa rambirambi kwa familia ya marehemu kutokana na msiba huo.


“Ni masikitiko makubwa kumpoteza Chama ambaye alilitumikia taifa naungana kumuombea marehemu na ninatoa pole kwa familia yake,wana familia ya mpira wa miguu ,ndugu na jamaa zake wa karibu pamoja na marafiki,Mungu aiweke mahala pema peponi roho ya Marehemu Athuman Juma Chama .Amina. Inna Lillah wa Innalillah Rajaun.”

Enzi za Uhai wake Marehemu Chama pamoja na kuichezea timu ya Taifa katika ngazi ya klabu alicheza kwenye vilabu vya Pamba na Yanga.
EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati. BOFYA HAPA KUJIUNGA NA INNOVATION FURSA CHALLENGE http://www.edusportstz.com ni fahari ya wasomaji
UNGANA NASI KUPITIA LIKI HIZI ILI KUTUMIWA HABARI POPOTE ULIPO


EDUSPORTSTZ NI FAHARI YA WASOMAJI

WEKA EMAIL YAKO:


Delivered by EDUSPOTSTZ
Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno
EDUSPORTSTZ