BEKI WA WEST BROM AWANIWA NA MAN CITY NA ARSENAL - EDUSPORTSTZ

Latest

BEKI WA WEST BROM AWANIWA NA MAN CITY NA ARSENAL


Meneja mpya wa West Brom Alan Pardew amesema klabu hiyo itamuuza tu iwapo itapata 'ofa bora zaidi'

Arsenal na Manchester City wanataka kumnunua beki wa West Brom Jonny Evans.

Meneja wa Arsenal Arsene Wenger anaaminika kuwa tayari kuomba klabu yake kutoa £25m kumnunua mchezaji huyo wa miaka 30 kutoka Ireland Kaskazini.

Arsenal wana nafuu kidogo kwani West Brom wanamtaka beki wa kushoto Mathieu Debuchy, 32, ambaye anatafuta fursa ya kuchezwa kikosi cha kwanza.

City wanataka mchezaji wa kujaza nafasi ya nahodha Vincent Kompany ambaye ameumia tena.

Klabu nyingine za Ligi ya Premia pia zinamtaka Evans lakini haziwezi kushindana na klabu ambazo zinacheza soka ya Ulaya.

Evans alijiunga na West Brom kutoka Manchester United kwa £6m Agosti 2015.
EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati. BOFYA HAPA KUJIUNGA NA INNOVATION FURSA CHALLENGE http://www.edusportstz.com ni fahari ya wasomaji
UNGANA NASI KUPITIA LIKI HIZI ILI KUTUMIWA HABARI POPOTE ULIPO


EDUSPORTSTZ NI FAHARI YA WASOMAJI

WEKA EMAIL YAKO:


Delivered by EDUSPOTSTZ
Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno
EDUSPORTSTZ


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz