BOCCO WA SIMBA NDO HABARI YA MJINI KWASASA - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Tuesday, 2 January 2018

BOCCO WA SIMBA NDO HABARI YA MJINI KWASASAUnaweza kusema mashabiki wa soka hawana kauli moja baada ya baadhi yao kumsifia mshambuliaji wa Simba, John Bocco kuwa anajituma sana.


Baada ya Bocco kufunga mabao mawili wakati Simba ikiimaliza Ndanda FC kwa mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara, mashabiki hasa wa Simba wanaonekana kufurahishwa na mwendo wa Bocco.
Katika mijadala ya makundi mbalimbali pia kupitia mtandao wa Instagram, mashabiki hao wa soka wameonyesha kufurahishwa na Bocco.


Wengi wameeleza pamoja na kufunga lakini amekuwa akicheza kwa juhudi kubwa na inapaswa kuwa mfano kwa wengine,
Lakini wako waliosema, Bocco anaonekana ana malengo hata kuliko wachezaji wengi wa kigeni kwa kuwa hataki kufeli.
Wakati wakimwagia sifa kibao, siku chache zilizpita, mashabiki walikuwa wakilalama kwamba Bocco anaonekana kutokuwa na msaada.Mara kadhaa, hadi uwanjani walikuwa wakipiga kelele kutaka Bocco ataolewe, madai kwamba hana msaada.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati http://www.edusportstz.com ni fahari ya wasomaji
UNGANA NASI KUPITIA LIKI HIZI ILI KUTUMIWA HABARI POPOTE ULIPO

EDUSPORTSTZ NI FAHARI YA WASOMAJI

WEKA EMAIL YAKO:


Delivered by EDUSPOTSTZ
Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno
EDUSPORTSTZ