BADNEWS:KOCHA WA MWADUI FC JUMA NTAMBI AMEFARIKI DUNIA USIKU WA KUAMKIA LEO - EDUSPORTSTZ

Latest

BADNEWS:KOCHA WA MWADUI FC JUMA NTAMBI AMEFARIKI DUNIA USIKU WA KUAMKIA LEO




Habari ya kushtusha na kusikitisha kwa mashabiki wa Mwadui na wapenzi wa mpira wa miguu nchini juu ya kifo cha kocha msaidizi wa Kikosi hicho Jumanne Ntambi ambaye amefariki dunia usiku wa kuamkia leo kutokana na kuzidiwa na Malaria yaliyokuwa yakimkabili.

Awali zilisambaa taarifa za kifo cha kocha huyo kwamba ameanguka bafuni majira ya saa 3 usiku na ndiyo sababu ya kufariki kwake, lakini sokaonline haikuwa mbali na habari hiyo usiku kuhakikisha unapatikana uhakika wa habari hiyo.

Katibu mkuu wa klabu hiyo ametuthibitishia majira ya saa 6 usiku kwamba ni kweli wamempoteza Mwalimu wao Msaidizi usiku huu (usiku wa kuamkia leo) kutokana na kuzidiwa na Malaria ambayo yalikuwa yanamsumbua mpaka kumpelekea kupoteza maisha.

Akiongea nasi katibu mkuu wa timu hiyo alisema “Hivi sasa tumetoka mochwari, marehemu alizidiwa majira ya saa 2 usiku na sisi tukamkimbiza hospitali lakini bahati mbaya ilipofika majira ya saa 3 marehemu akafariki, Marehemu alikuwa anasumbuliwa na Malaria siku chache zilizopita lakini alikuwa hajagundua kuwa ana presha na ilimchukua muda kidogo mpaka alipogundua kuwa presha imebadilka, hivyo tumefanya jitihada imeshindikana”.

Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya kocha Jumanne Ntambi, watanzania na wapenda soka kwa ujumla tutakukumbuka kwa mchango wako kwenye soka la Tanzania. EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati. BOFYA HAPA KUJIUNGA NA INNOVATION FURSA CHALLENGE http://www.edusportstz.com ni fahari ya wasomaji
UNGANA NASI KUPITIA LIKI HIZI ILI KUTUMIWA HABARI POPOTE ULIPO

EDUSPORTSTZ NI FAHARI YA WASOMAJI

WEKA EMAIL YAKO:


Delivered by EDUSPOTSTZ
Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno
EDUSPORTSTZ


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz