AZAM FC WALIBAKIZA KOMBE LA MAPINDUZI TANZANIA - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

DOWNLOAD AJIRA DAILY HAPA

Sunday, 14 January 2018

AZAM FC WALIBAKIZA KOMBE LA MAPINDUZI TANZANIA


Image result for AZAM FC

Mbele ya Rais wa Zanzibar, Ali Mohammed Shein aliyekuwa mgeni rasmi, Azam FC wametimiza kile walichokitaka Watanzania wengi baada ya kubeba ubingwa wa Kombe la Mapinduzi.

Kikosi cha Azam FC kimeshinda kwa mikwaju 4-3 ya penalti dhidi ya URA ya Uganda katika mechi ya fainali ya Mapinduzi.

URA ilikuwa kama imekuwa kiboko ya Watanzania, kwa kuwa ndiyo iliitoa Simba katika michuano ya Mapinduzi, baadaye ikafanya hivyo kwa kuing'oa Yanga pia.

Lakini, tayari ilikuwa imeishinda Azam FC katika hatua za makundi. Lakini leo mambo yalikuwa magumu baada ya dakika 90 kwisha kwa sare ya bila mabao.

Dakika za nyongeza bado mambo yalikuwa magumu baada ya sare ya 0-0.

Walipoingia katika mikwaju ya penalti, kipa wa Azam FC, Razack Abarola ndiye alikuwa shujaa kwa kupangua mikwaju miwili ya Waganda hao
EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati. BOFYA HAPA KUJIUNGA NA INNOVATION FURSA CHALLENGE http://www.edusportstz.com ni fahari ya wasomaji
UNGANA NASI KUPITIA LIKI HIZI ILI KUTUMIWA HABARI POPOTE ULIPO


EDUSPORTSTZ NI FAHARI YA WASOMAJI

WEKA EMAIL YAKO:


Delivered by EDUSPOTSTZ
Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno
EDUSPORTSTZ