WALIOSAJILIWA RUVU SHOOTING HAWA HAPA - EDUSPORTSTZ

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Monday, 18 December 2017

WALIOSAJILIWA RUVU SHOOTING HAWA HAPA
Ruvu Shooting yasajili WATANO, WATAMU dirisha dogo.

Katika usajili wa dirisha dogo, klabu ya Ruvu Shooting imesajili wachezaji watano vijana ili kukiongezea nguvu kikosi katika duru ya lala salama ya Ligi kuu ya Voda com Tanzania bara 2017/18.

Wachezaji waliosaini mkataba kutumika katika kikosi cha Ruvu Shooting ni kiungo namba nane Hamis Salehe Maulid na Adam Ibrahim Abdallah ambaye ni winga wa kulia.

Wengine ni washambuliaji Gidion Brown Benson na Alinanuswe Martin Mwaisemba na beki Rajab Zahir Mohamed.

Wachezaji hao tayari wako kambini wakiendelea na mazoezi isipokuwa Zahir ambaye ataripoti kambini muda wowote kuanzia sasa.
EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati http://www.edusportstz.com ni fahari ya wasomaji
Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno

No comments:

Post a Comment