YAJUE MAMBO MATANO YANAYOTISHIA USALAMA KWA NCHI ZA AFRKA MASHARIKI - EDUSPORTSTZ

Latest

YAJUE MAMBO MATANO YANAYOTISHIA USALAMA KWA NCHI ZA AFRKA MASHARIKI



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Augustine Mahiga amesema kuna aina nne za mambo yanayotishia usalama katika nchi za Afrika Mashariki.

Akitaja mambo hayo, Balozi Mahiga amesema ni ugaidi, uharamia, na majanga mengine kama matetemeko ya ardhi na masuala ya kisiasa.

Balozi Mahiga amesema hayo juzi (Ijumaa) wakati akifunga mafunzo ya ‘Ushirikiano Imara 2017’, jijini Dar es Salaam, ambayo nchi za Afrika Mashariki zimeshiriki ikiwemo na Tanzania.

Amesema licha ya mambo hayo kuwa tishio, bado majeshi ya usalama yapo imara, na Tanzania mpaka sasa haijafikia hatua ambayo inatishia amani.

Akizungumzia mafunzo hayo, Balozi Mahiga amesema mafunzo hayo yanaleng la kudumisha uzalendo na kubadilishana mawazo na nchi nyingine za Afrika Mashariki.

“Zoezi hili ni la muhimu sana na sehemu ya itifaki. Mwaka jana yalifanyika nchini Kenya. Leo ni fursa ya uongozi wa juu kabisa katika majeshi ya Afrika Mashariki kukaa pamoja na kufanya mazoezi pamoja na Tanzania tumekuwa wenyeji.” amesema Balozi Mahiga.

Naye Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Luteni Jenerali James Mwakibolwa amesema lengo la mafunzo hayo ni kubadilishana uzoefu na kuongeza ufanisi na weledi katika majeshi.

Chanzo:HabariLEO

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati http://www.edusportstz.com ni fahari ya wasomaji
Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz