VICTOR WANYAMA KURUDI RASMI KATIKA MAZOEZI NA KIKOSI CHAKE CHA TOTTENHAM - EDUSPORTSTZ | Habari za Ajira, Mapenzi, Michezo, Elimu, Kilimo, Technology, Siasa na Mziki,

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Friday, 22 December 2017

VICTOR WANYAMA KURUDI RASMI KATIKA MAZOEZI NA KIKOSI CHAKE CHA TOTTENHAM

Kiungo wa kati wa Tottenham Victor Mugubi Wanyama katika mechi iliopita

Kiungo wa kati wa Tottenham Victor Wanyama amerudi katika mazoezi kufuatia jeraha la goti na huenda akarudi katika kikosi cha Pochetino kulingana na meneja huyo.

Wanyama hajaichezea Spurs tangu timu hiyo ishindwe 2-1 na Chelsea mnamo mwezi Agosti.

Pochettino ambaye kikosi chake kitacheza mechi ya ugenini dhidi ya Burnley siku ya Jumamosi , anasema kuwa Spurs imemkosa sana mkenya huyo mwenye umri wa miaka 26 msimu huu.

''Ni hisia nzuri kutoka kwake'', alisema raia huyo wa Argentina.''Tutaona ni lini atashirikishwa tena''.

''Msimu uliopita alikuwa mchezaji muhimu sana kwetu.Na msimu huu , ni kweli.Katika hali ambayo unatakikana kuwa na nguvu tumemkasa mchezaji kama huyu''.

Victor Wanyama huwa ana kisasi na Arsenal?

''Itakuwa vyema iwapo haraka iwezekanavyo atashiriki tena kwa sababu ni mchezaji mzuri na muhimu sana''.

Wanyama ambaye alikosa mechi mbili pekee za ligi ya Uingereza wakati Tottenham ilipomaliza ya pili msimu uliopita alipata jereha hilo wakati wa dirisha la uhamisho lililopita.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati http://www.edusportstz.com ni fahari ya wasomaji
Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno

No comments:

Post a Comment