-->

Type something and hit enter

On

Mesut Ozil

Mesut Ozil 29, angependa kuhamia Manchester United badala ya Barcelona ikiwa ataondoka Arsenal. (Daily Mail)

Ajenti wa Ozil ameimbia Barcelona kuwa ni lazima wafanye uamuzi ikiwa watamsaini mchezaji huyo au la katika kipindi cha wiki mbili zinazokuja (Mundo Deportivo)

Nahodha wa Barcelona Andres Iniesta anasema mshambuliaji wa Liverpool Philippe Coutinho, 25, atakuwa muhimu ikiwa watamuendea mwezi Januari. (Goal)Ronaldo

Ronaldo anawaomba ushauri mawakili wake kujaribu kuondoka Real Madrid. (El Chiringuito kupitia Daily Express)

Willian amewahakikishia mashabiki wa Chelsea kwamba hataondoka mwezi Januari, baada mchezaji huyo wa safu ya kati kuhusishwa na kuelekea huko Manchester United na Barcelona. (Evening Standard)

Newcastle wanatathmini kumpa ofa mshambuliaji wa Liverpool Danny Ings, 25 na mlinzi wa Manchester United Luke Shaw, 22, mwezi ujao. (Daily Star)Danny Ings

Jose Mourinho amemuorodhesha mchezaji wa safu ya kati wa Inter Milan raia wa Ureno Joao Mario, 24, kama atakayechukua mahala pake Henrikh Mkhitaryan huko Manchester United. (Corriere dello Sport kupitia Mirror)

Kipa wa AC Milan Gianluigi Donnarumma, 18, ametaka mkataba wake mpya kufutwa huko Real Madrid wakati Paris St-Germain wakitaka kumsaini. (Gazzetta dello Sport)

Sporting Lisbon wanataka kumchukua mshambuliaji wa Leicester Islam Slimani, 29, kutoka Ureno kwa mkopo mwezi Januari. (A Bola, kupitia Talksport)EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati http://www.edusportstz.com ni fahari ya wasomaji
Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno
Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB

Click to comment