HATIMAYE YAYA TOURE ATENGUA KAULI YAKE MWENYEWE - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

DOWNLOAD AJIRA DAILY HAPA

Thursday, 28 December 2017

HATIMAYE YAYA TOURE ATENGUA KAULI YAKE MWENYEWE
Miezi 15 iliyopita kiungo wa klabu ya Manchester City na timu ya taifa ya Ivory Coast Yaya Toure aliutangazia ulimwengu kwamba anaachana na timu ya taifa ya Ivory Coast na kuelekeza nguvu klabuni.

Lakini sasa kiungo huyo ametengua kauli yake na kuamua kurejea tena katika timu ta taifa ya Ivory Coast katika kipindi hiki ambacho hana uhakika wa kupata namba katika kikosi cha kwanza cha Pep Gurdiola.

Wakala wa Yaya Toure bwana Dimitri Seluk amesema kiungo huyo amerejea katika timu ya taifa ya Ivory Coast sababu bado anaona anahitaji kushinda kombe lingine akiwa na timu ya taifa na sasa amerudi kulitafuta.

Yaya mwenyewe akielezea sababu kwanini amerudi katika timu ya taifa alisema “nalipenda sana taifa langu na nduo sababu nimerudi kama nitahitajika, ningependa kukisaidia kizazi kijacho kwa uzoefu nilionao”.

Yaya Toure alikuwepo katika kikosi cha timu ya taifa ya Ivory Coast kilichoshinda michuano ya mataifa ya Africa mwaka 2015 na alifanikiwa kuichezea Ivory Coast mechi zaidi ya 100 huku mchezo wake wa mwisho ulikuwa September 2016.

Wakati huo huo wakala wa mchezaji huyo amesema Yaya hana mpango wa kuondoka Man City mwezi January kama inavyotajwa kwani ana mpango wa kushinda kombe lingine la EPL na klabu hiyo.
EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati http://www.edusportstz.com ni fahari ya wasomaji

UNGANA NASI KUPITIA LIKI HIZI ILI KUTUMIWA HABARI POPOTE ULIPO


EDUSPORTSTZ NI FAHARI YA WASOMAJI

WEKA EMAIL YAKO:


Delivered by EDUSPOTSTZ
Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno
EDUSPORTSTZ