BAVICHA WAFUNGUKA KUHUSU WEMA SEPETU - EDUSPORTSTZ | Habari za Ajira, Mapenzi, Michezo, Elimu, Kilimo, Technology, Siasa na Mziki,

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Monday, 4 December 2017

BAVICHA WAFUNGUKA KUHUSU WEMA SEPETU

Wasema Wema Hakuwa mwanachama Chadema bali Alikuwa ni Shabiki Tu
Umoja wa Vijana wa Chadema (Bavicha) umesema mrembo huyo wa Tanzania mwaka 2006, Wema Abraham Sepetu hakuwahi kuwa mwanachama wala kukabidhiwa jukumu lolote katika operesheni za chama hicho kikuu cha upinzani kwani alikuwa shabiki.

Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Patrick Ole Sosopi amesema hayo juzi baada ya kutangazwa kurithi nafasi ya aliyekuwa Mwenyekiti, Patrobas Katambi ambaye amehamia Chama Cha Mapinduzi mwezi uliopita.


“Wema alikuwa shabiki wa Chadema na Chadema ina wafuasi wa namna mbalimbali. Wapo tunaowafahamu na tusiowafahamu. Wema hakuwa chochote ndani ya Chadema. Wema hakuwahi kufanya ‘movement’ yoyote. Msiwe mnasema amerudi, kwani anatoka wapi?"- Ole Sosopi.
Aliongeza; “Wema hakuwahi kupewa kadi yoyote ya Chadema. Alikuja kwa matatizo yake na ameondoka kwa matatizo yake lakini hakuwa na sifa hata ya kuwa mjumbe wa nyumba kumi. Wema ameondoka peke yake, wacha waondoke".

Ole Sosopi aliyeteuliwa na Kamati ya Utendaji ya Bavicha kuwa kiongozi wake, alisema kwa sasa Chadema inapitia kipindi muhimu kitakachoiimarisha.

Hata hivyo Ole Sosopi aliongeza kwamba CHADEMA wameweka mipango katika katiba kuhusiana na watu wanaohama wakitaka kurudi ndani ya chama hicho hawatakubaliwa mpaka wafanyiwe uchunguzi wa kutosha kama dhamira yao ni njema kwani wao si kama daladala ambalo unapanda, unashuka ili mradi uwe na nauliinakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati http://www.edusportstz.com ni fahari ya wasomaji
Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno

No comments:

Post a Comment