-->

Type something and hit enter

On
Pakua App MPYA ya 'EDUSPORTSTZ NEWS-(Lite Version)' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB
Chama cha ACT -Wazalendo kimesitisha mchakato wa uchaguzi mdogo wa majimbo matatu na kata sita kikisubiri uamuzi wa Kamati Kuu.


Kaimu Katibu Mkuu wa ACT -Wazalendo, Dorothy Semu katika taarifa kwa makatibu wa mikoa ya Tanga, Tabora, Ruvuma, Arusha, Iringa, Pwani na Singida amesema kamati ya uongozi ya chama hicho katika kikao cha dharura cha Desemba 8,2017 mjini Dar es Salaam imetoa maelekezo mawili.

Amesema mosi; kwamba viongozi wa mikoa, majimbo na kata zenye uchaguzi wasitishe mchakato wa kushiriki uchaguzi mdogo.

Pili; Dorothy amesema mikoa itapokea maelekezo kuhusu uchaguzi mdogo kutoka ofisi ya katibu mkuu baada ya Kamati Kuu ya ACT -Wazalendo kukutana hivi karibuni.

Amesema kamati ya uongozi ya Taifa imefikia uamuzi huo kutokana na hali iliyotokea wakati wa uchaguzi mdogo wa kata 43 uliofanyika Novemba 26,2017.

Baadhi ya yaliyojitokeza amesema ni pamoja na kubinywa kwa demokrasia na vurugu zilizotokea katika maeneo mbalimbali.

“Hivyo, kamati kuu itafanya tathmini ya uchaguzi mdogo wa kata 43 na kutoa mwelekeo wa chama juu ya uchaguzi wa majimbo matatu na kata sita unaoanza mchakato Desemba 12,2017 na kukamilika Januari 13,2018,” amesema.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati http://www.edusportstz.com ni fahari ya wasomaji
Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno
Pakua App MPYA ya 'EDUSPORTSTZ NEWS-(Lite Version)' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB

Click to comment
 
Blog Meets Brand