SAMMATA MBIONI MWA TAJI LA MCHEZAJI BORA AFRIKA 2017 - EDUSPORTSTZ

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Wednesday, 1 November 2017

SAMMATA MBIONI MWA TAJI LA MCHEZAJI BORA AFRIKA 2017


Shirikisho la soka barani Afrika limetoa orodha ya wachezaji 30 watakaowania taji la mchezaji bora wa soka barani Afrika mwaka huu.

Mshambuliaji wa Gabon Pierre Erick Aubameyang aliyeshinda mwaka 2015 ameorodheshwa pamoja na nyota kadhaa wanaosakata dimba barani Ulaya kama vile mshambuliaji wa Senegal na Liverpool Sadio Mane ambaye alikuwa katika nafasi ya tatu 2016.Pia mbwana Ali Samatta amewekwa katika orodha hiyo


Mshindi wa mwaka 2016 Riyad Mahrez wa Algeria hakuorodheshwa katika orodha hiyo.

Kati ya wachezaji 30 waliorodheshwa ni saba pekee ambao hawachezi soka yao barani Ulaya, huku kipa wa Misri aliye na umri wa miaka 44 pia akiorodheshwa.

Kipa huyo wa miaka mingi anacheza soka yake katika klabu ya Al-Taawoun nchini Saudi Arabia.

Kwengineko Mahrez ameshindwa kuonyesha umahiri wake ambao alionyesha wakati alipokuwa kiungo muhimu wa klabu ya Leicester na kuiwezesha kushinda ligi ya Uingereza

Wachezaji wanne wanaosakata soka yao Afrika wameorodheshwa kuwania taji la mchezaji bora wa bara Afrika mbali na mchezaji bora anayesakata soka barani humu.

Wachezaji hao ni mchezaji wa Tunisia Ali Maaloul (Al Ahly), mchezaji wa Afrika Kusini Percy Tau, Kipa wa Uganda Dennis Onyango (wote wa Mamelodi Sundowns) na Fackson Kapumbu wa Zambia anayeichezea klabu ya (Zesco United).

Washindi wa mataji hayo watatangazwa katika mji mkuu wa Ghana Accra mnamo tarehe 4 mwezi January 2018.

Kura zitakazopigwa na makocha, wakurugenzi wa kiufundi kutoka mataafa mbali mbali pamoja na wanachama wa kiufundi wa Caf na kamati endelvbu mbali na jopo la waandishi zitabaini washindi.
Orodha ya wachezaji wa taji la mchezaji bora Afrika


like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika Propellerads

For Booking>>>CALL>>>

Voda: +255757441463

JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI
No comments:

Post a Comment