MBWA AINGIA UWANJAN MECHI IKIENDELEA NA KUKIMBIA NA MPIRA - EDUSPORTSTZ | Habari za Ajira, Mapenzi, Michezo, Elimu, Kilimo, Technology, Siasa na Mziki,

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Wednesday, 1 November 2017

MBWA AINGIA UWANJAN MECHI IKIENDELEA NA KUKIMBIA NA MPIRA


Mbwa asimamisha mechi Bolivia Akimbia na Mpira Katikati ya Mechi

Mbwa wa polisi amezua taharuki wakati alipoingia uwanjani na kukimbia na mpira wa mchezo wa kati ya Blooming dhidi ya Nacional de Potosi waLigi Kuu Bolivia.

Mbwa huyo wa polisi alifanikiwa kutoka mikononi mwa askari aliyekuwa amemshika na kuingia uwanjani wakati mechi ikiendelea kabla ya kuung’ata mpira na kukimbia.

Kitendo hicho cha mbwa kukimbia na mpira ukiwa mdomoni mwake kilisababisha mechi kusimama kwa sekunde 40.

Askali walianza kumkimbiza mbwa huyo uwanjani jambo lililofanya mashabiki wa watazamaji kupata burudani ya aina yake.

Mwisho mchezaji Alejandro Quintana anayechezea Blooming alifanikiwa kumkata mbwa huyo na mechi kuendelea.

Mwisho wa mechi hiyo Blooming ilifanikiwa kushinda kwa mabao 4-2, lakini mbwa huyo wa polisi ndiye aliyeshika vichwa vya habari.

 like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika Propellerads

For Booking>>>CALL>>>

Voda: +255757441463

JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI
No comments:

Post a Comment