TAZAMA SAFARI YA MESSI KUELEKEA MECHI YA 600 - EDUSPORTSTZ

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Saturday, 4 November 2017

TAZAMA SAFARI YA MESSI KUELEKEA MECHI YA 600


 MESSI KATIKA MCHEZO WA 600
Messi alianza kuichezea Barcelona msimu wa 2004/05 chini ya kocha Frank Rijkaard ambaye alimpandisha kutoka La Masia na kumwamini akiwa na miaka 17 pekee. Messi chini ya Rijkaard alicheza mechi 110 katika misimu ya 2004/05, 2005/06, 2006/07 na 2007/08.


Hata hivyo Messi alipata nafasi zaidi kwenye kikosi cha kwanza chini ya kocha Pep Guardiola kuanzia msimu wa 2008/09. Chini ya Guardiola Messi aliacheza mechi 218 kwenye misimu ya 2008/09, 2009/10, 2010/11 na 2011/12.

Baadae alicheza mechi 50 chini ya Tito Vilanova msimu ya 2012/13, kabla ya kucheza mechi 46 chini ya Tata Martino msimu wa 2013/14. Messi alicheza mechi nyingi tena chini ya Luis Eanrique misimu ya 2014/15, 2015/16, 2016/17 jumla ya michezo 158.

Hivi sasa Messi yupo chini ya kocha Ernesto Valverde ambapo tayari amecheza mechi 16 na kufanya afikishe michezo 599 na endapo leo ataanza kwenye mechi dhidi ya Sevilla atafikisha michezo 600.

like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika Propellerads

For Booking>>>CALL>>>

Voda: +255757441463

JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI
No comments:

Post a Comment