MKWASA:NGOMA AKIREJEA LAZIMA TUMCHUKULIE HATUA ZA KINIDHAMU - EDUSPORTSTZ

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Thursday, 9 November 2017

MKWASA:NGOMA AKIREJEA LAZIMA TUMCHUKULIE HATUA ZA KINIDHAMU

Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa amesisitiza kuwa ni lazima wampe adhabu mshambuliaji wao Mzaimbabwe, Donald Ngoma kwa utovu wa nidhamu.Hayo, aliyasema katika mazoezi ya jana asubuhi yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam chini kocha msaidizi, Shadrack Nsajigwa.


Taarifa zinasema kuwa, mshambuliaji huyo aliondoka nchini na kurejea nyumbani kwao Zimbabwe bila ya kutoa taarifa kwa viongozi wake.


Mkwasa alisema, hawana taarifa za kuondoka kwa mshambuliaji huyo aliyekuwepo nje ya uwanja kwa muda wa wiki tatu na nusu kutokana na kusumbuliwa na majeraha ya goti.


“Hatuna taarifa za kuondoka kwa Ngoma na kama ameondoka basi atakuwa kafanya makosa kwani hakutoa taarifa kwa uongozi.“Hivyo, kama akirejea nchini na kujiunga na klabu ni lazima tumchukulie hatua za kinidhamu ikiwemo adhabu kwa kitendo alichokifanya,” alisema Mkwasa.


Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno

No comments:

Post a Comment