LIONEL MESSI AFIKIA REKODI YA ROBERTO CARLOS - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

DOWNLOAD AJIRA DAILY HAPA

Thursday, 23 November 2017

LIONEL MESSI AFIKIA REKODI YA ROBERTO CARLOS





Cesc Fabregas alifunga moja ya bao wakati Chelsea ikiwaua Quarabag bao 4 yaliyoipeleka Chelsea 16 bora na goli lake la leo linamfanya kuwa Mhispania wa 4 kufunga mabao 20+ katika Champions League baada ya Fernando Torres,Fernando Morientes na Raul.

Mshambuliaji wa Kibrazil Neymar alifunga mabao mawili leo zidi ya Celtic huu ulikuwa mchezo wake wa 200 tangu afike barani Ulaya na mabao ya leo yamemfanga kufikisha mabao 201 katika mechi hizo.

Mabao mawili ya leo ya Neymar yamemfanya kufikisha jumla ya magoli 27 katika mechi 45 za Champions League ambapo ni Mbrazil mmoja tu Ricardo Kaka ndio mwenye idadi kubwa kuliko Neymar katika michuano hiyo(mabao 30).

Wakati Barcelona wakitoka sare na Juventus, mshambuliaji wa klabu ya Argentina Lioneil Messi alikuwa akicheza mchezo wake wa 120 na sasa anakuwa amecheza idadi sawa na beki wa zamani wa Brazil Roberto Carlos katika michuano hiyo(ndio Waamerica Kusini wanoongoza kwa mechi nyingi).

Suluhu ya leo ya Barcelona imefanya hii leo kuwa mara ya kwanza kwa klabu hiyo kushindwa kupata bao katika mechi mbili mfululizo za Champions League katika hatua ya makundi tangu washindwe kufanya hivyo mwaka 2000 lakini wamefuzu kwenda 16 bora.

Matokeo mengine Atletico waliifunga Roma bao 2 kwa nunge kwa mabao ya Gemmeiro na Antoine Griezman na kufufua matumaini ya Atletico kusonga mbele huku Fc Bayern wakiifunga Anderchelt 2 kwa 1.
EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati http://www.edusportstz.com ni fahari ya wasomaji
Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno