KOCHA MSAJIGWA ATETA JINSI SIMBA ILIVYOWAPA KIBURI - EDUSPORTSTZ

Latest

KOCHA MSAJIGWA ATETA JINSI SIMBA ILIVYOWAPA KIBURI


 simba na yanga

KOCHA Msaidizi wa Yanga, Shadrack Nsajigwa ametamba kuwa, soka safi walilocheza dhidi ya Simba, limewaondoa hofu ya kuivaa Singida United leo Jumamosi, hivyo wana uhakika wa ushindi.

Yanga inacheza na Singida United mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Namfua mkoani Singida.
Timu hizo zinacheza zikiwa na kumbukumbu ya kutoka sare ya bao 1-1 katika mechi ya kirafiki kujiandaa na msimu huu iliyochezwa Agosti mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Nsajigwaa amesema kuwa, kama waliweza kufika langoni na kutengeneza nafasi nyingi za kufunga dhidi ya Simba, basi ni ishara tosha kikosi chao kipo fiti kupata matokeo mazuri dhidi ya Singida United.
Nsajigwa alisema, mechi na Singida United siyo nyepesi kwao, hivyo watapambana katika mchezo huo kuhakikisha wanavuna pointi tatu ili wapande kukaa kileleni mwa ligi.

Wachezaji wa timu ya Singida United wakifanya mazoezi.

Yanga ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 16 sawa na Simba lakini imezidiwa mabao ya kufunga, lakini Singida United ni ya sita ikiwa na pointi 13 katika mechi nane kama Yanga.

“Tulicheza vizuri bila nyota kadhaa dhidi ya Simba na kufika langoni na kutengeneza nafasi nyingi za mabao ni ishara tosha kikosi chetu kipo fiti na kombinesheni zimeanza kuelewana.

“Hiyo ni salamu tosha kwa wapinzani wetu tutakaokutana nao katika mechi zijazo za ligi kuu kuwa tupo fiti kuchukua pointi tatu ili tufanikishe malengo yetu,” alisema Nsajigwa.

Katika msafara wa timu hiyo ulioelekea Singida juzi, kivutio kikubwa kilikuwa ni kiungo mkabaji raia wa DR Congo, Papy Kabamba Tshishimbi ambaye sehemu kubwa ya walipopita alishangiliwa na mashabiki walioomba pia kupiga picha naye.

 like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika Propellerads

For Booking>>>



CALL>>>

Voda: +255757441463

JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI










Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz