KAULI YA HANS POPPE YAPINGWA NA MASHABIKI WA SIMBA - EDUSPORTSTZ | Habari za Ajira, Mapenzi, Michezo, Elimu, Kilimo, Technology, Siasa na Mziki,

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Tuesday, 14 November 2017

KAULI YA HANS POPPE YAPINGWA NA MASHABIKI WA SIMBA


HANS POPPE:SISI HATUWEZI KUENDELEA KUMLIPA MTU AMBAYE HACHEZIMashabiki wa Simba wamemshukia Mwenyekiti wao wa Kamati ya Usajili, Zacharia Hans Poppe.


Mashabiki hao kupitia mitandao mbalimbali wakionyesha wazi kupinga kauli yake dhidi ya beki Shomari Kapombe.


Kapombe ni majeruhi lakini Hans Poppe alionyesha kushangazwa na Kapombe kutorejea uwanjani huku akisisitiza amepona.


Hans Poppe alikwenda mbali zaidi na kutishia akisema arejee acheze au aende kwa kuwa hawawezi kuendelea kumlipa mtu mshahara akiwa nje.


Mashabiki hao wamemtaka Hans Poppe kuwa muungwana hasa baada ya Kapombe kujibu akisema bado ni majeruhi na hawazi kucheza,.


Kapombe amesisitiza kama Simba wako tayari kuvunja mkataba hana tatizo.Mashabiki wengine wamemshambulia Hans Poppe kwa lugha chafu wakidai si kauli ya kiongozi anayeweza kuzungumza hivyo badala ya kuzungumza na mchezaji au kuchukua hatua.


Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno

No comments:

Post a Comment