ITALIA HATARINI KUKOSA KUFUZU KOMBI LA DUNIA - EDUSPORTSTZ

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Saturday, 11 November 2017

ITALIA HATARINI KUKOSA KUFUZU KOMBI LA DUNIA


Sweden walimaliza juu ya Uholanzi kwa wingi wa mabao kufika hatua ya muondoano


Meneja wa Italia Giampiero Ventura amesema taifa lake litahitaji kucheza kwa ustadi sana mechi yao ya marudiano katika mechi za muondoano wa kufuzu dhidi ya Sweden kuzuia kukosa kufuzu kwa Kombe la Dunia mara ya kwanza tangu 1958.

Sweden walishinda mechi ya kwanza 1-0 uwanjani Friends Arena, bao pekee likitokana na kombora la Jakob Johansson la hatua 20 kutoka kwenye goli ambalo lilijipinda baada ya kumgonga Daniele de Rossi.

Sweden walicheza vyema zaidi kipindi cha kwanza, lakini Azzurri waliimarika kiasi kipindi cha pili. Lakini bado hawakuweza kuondoka na chochote ila masikitiko kutoka kwa mechi hiyo.

Matteo Darmian ndiye aliyekaribia zaidi kusawazisha lakini kombora lake liliugonga mlingoti wa goli.

Italia, ambao watakuwa bila Marco Verratti ambaye anatumikia marufuku, watahitaji kushinda mechi ya marudiano Jumatatu uwanjani San Siro kufika Kombe la Dunia Urusi mwaka ujao.

Ventura alisema: "Matokeo haya yanaumiza. Natumia kwamba mjini Milan maafisa wa mechi watatupatia kile ambacho waliwapatia hapa.

"Katika mechi muhimu kama hii tulihitaji maamuzi yasiyoegemea upande wowote. Lakini sasa lililo muhimu zaidi ni matokeo tu.

"Ni lazima tufanye kila juhudi Milan. San Siro lazima ituinue kiasi lakini pia tutahitajika kucheza vyema zaidi kwa ajili ya mashabiki wetu."Kipa wa Sweden Robin Olsen alihitajika kuokoa mpira mara mbili pekee

Sweden, waliomaliza juu ya Uholanzi kundini kwa wingi wa mabao na kupata nafasi ya pili ya kujaribu kufuzu kupitia mechi za muondoano walionekana kuwa na matumaini tangu kipenga cha kwanza kilipopulizwa.

Sweden - walioshindwa na Italia katika Euro 2016 - watahitajika tu kuhakikisha hawafungwi na Italia mechi hiyo ya Italia kufuzu kwa Kombe la Dunia mara ya kwanza tangu 2006.
Kwa kuwa sheria ya mabao ya ugenini inatumika mechi za muondoano, Sweden wakifunga bao moja San Siro itakuwa na maana kwamba Azzurri watahitaji kufunga mabao matatu kufuzu.Matumaini ya Gianluigi Buffon kucheza Kombe la Dunia mara ya sita yamo mashakaniNahodha wa Sweden Andreas Granqvist alikuwa mchezaji bora wa mechiFollow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno

No comments:

Post a Comment