HII NDIO REKODI ILIYOWEKWA NA LUKAKU KWENYE TIMU YA UBELGIJI - EDUSPORTSTZ | Habari za Ajira, Mapenzi, Michezo, Elimu, Kilimo, Technology, Siasa na Mziki,

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Wednesday, 15 November 2017

HII NDIO REKODI ILIYOWEKWA NA LUKAKU KWENYE TIMU YA UBELGIJI
Mshambuliaji wa Manchester United Romelu Lukaku amekuwa mchezaji wa Ubelgiji ambaye ameweka rekodi ya ufungaji mabao mengi kwa timu ya taifa hilo.


Vijana hao wa Roberto Martinez waliifunga Japan bao 1-0 huko Brugge.

Lukaku , 24, alifunga goli la 31 kwa nchi yake pale alipomalizia krosi safi kutoka kwa Nacer Chadli aliyoiingiza wavuni kwa kutumia kichwa.

Lukaku alikuwa ametoshana na Bernard Voorhoof na Paul van Himst walipokuwa na magoli 30 kila mmoja wiki iliyopita.

Ubelgiji waliendeleza msururu wao wa kutoshindwa hadi mechi 15.Image captionLukaku alifunga mabao yake ya kwanza ya kimataifa akichezea Ubelgiji nchini Urusi mwaka 2010

Mara yao ya mwisho kushindwa ilikuwa mikononi mwa Uhispania mechi ya kirafiki Septemba 2016.

Kwengineko, Uholanzi walipata ushindi wao wa pili tangu kukosa nafasi ya kushiriki katika Kombe la Dunia nchini Urusi walipopokeza Romania kichapo cha magoli 3-0 huko Bucharest.

Mshambuliaji wa zamani wa Liverpool Ryan Babel alifunga bao lake la kwanza la kimataifa tangu mwezi Mei 2008, pamoja na mchezaji mwenza Memphis Depay na Luuk de Jong.

Mabingwa wa Euro 2016 Ureno walitoka sare 1-1 na Marekani, wakicheza bila nyota wao Cristiano Ronaldo. Vitorino Antunes alikomboa bao lililokuwa limefungwa na Mmarekani Weston McKennie mapema mwenye mechi Leiria.

Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno

No comments:

Post a Comment