HALI YA MBWANA SAMATTA YATIA FARAJA - EDUSPORTSTZ | Habari za Ajira, Mapenzi, Michezo, Elimu, Kilimo, Technology, Siasa na Mziki,

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Thursday, 16 November 2017

HALI YA MBWANA SAMATTA YATIA FARAJA

 SAMATTA
HABARI nzuri kwa Watanzania na wapenzi wote wa soka ni kwamba, straika wa Genk ya ubelgiji na nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta ameanza kutembea mwenyewe bila msaada wa magongo au fimbo , aliyokuwa anatumia baada ya kufanyiwa upasuaji wiki iliyopita. Samatta ambaye aliukosa mchezo wa kirafiki wa Taifa Stars dhidi ya Benin wiki iliyopita matokeo yakiwa sare ya 1-1. Alipata maumivu ya goti la mguu wa kulia alipokuwa anaitumikia klabu yake Genk na jopo la madaktari wake, wakaamuru afanyiwe upasuaji ambao ulifanikiwa kwa kiasi kikubwa.

 Amesema: "Leo nimeacha kutumia fimbo za kutembelea."Katika kuzihirisha kuwa hali yake inaendelea vizuri, Samatta ametupia video yake kwenye mtandao wa Facebook, ikionyesha anatembea na gongo, baadaye akaliweka kando na kuanza kutembea kamili kwa miguu miwili kwa ukakamavu bila msaada.
Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno

No comments:

Post a Comment