BUSUNGU,MACHAKU WATIMULIWA KAMBINI, KISA HIKI HAPA - EDUSPORTSTZ

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Friday, 3 November 2017

BUSUNGU,MACHAKU WATIMULIWA KAMBINI, KISA HIKI HAPA

Mshambuliaji asiyeisha vituko Malimi Busungu na kiungo mshambuliaji wa Lipuli FC ya Iringa, Salum Machaku wametimuliwa kwenye kambi ya timu hiyo.Hiyo, ikiwa ni siku chache kabla ya mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Mwadui FC itakayochezwa kwenye Uwanja wa Samora mkoani Iringa.

Busungu alijiunga na Lipuli kwenye msimu huu akitokea Yanga baada ya mkataba wake kumalizika huku Machaku aliyewahi kuichezea akiwa ni mmoja wa nyota walioipandisha timu hiyo.

Taarifa zilizopatikana zimeeleza wachezaji hao wametimuliwa kutokana na nidhamu mbovu waliyoionyesha ndani ya timu.

Mtoa taarifa huyo alisema, kikubwa ni ulevi uliopindukia, kutolala kambini mara baada ya mechi za ligi kumalizika, hivyo katika kutengeneza nidhamu ya timu,uongozi umefikia maamuzi ya kuwatimua licha ya uwezo na uzoefu wao mkubwa waliokuwa nao.

Aliongeza kuwa, uongozi huo umetangaza kutokuwa na wachezaji hao kwa hivi sasa na tayari wameondolewa kambini kwa muda wa siku tano huku wachezaji wengine wakiendelea na maandalizi ya mchezo dhidi ya Mwadui.

“Wamekuwa wakifanya vitendo hivyo vya ulevi mara tu baada ya mechi ya ligi, sisi viongozi tumeamua kuwa hatutakuwa na wachezaji hao katika kipindi hiki,” alisema mtoa taarifa huyo.

Walipotafutwa wachezaji wenyewe hawakuweza kupatikana hadi tunaingia mitamboni lakini alipotafutwa kocha wa timu hiyo, Selemani Matola juu ya suala hilo alisema kwa ufupi: “Hao wachezaji hawapo kambini kutokana na utovu wa nidhamu, ukitaka kujua sababu zaidi watafute viongozi.”

 like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika Propellerads
For Booking>>>
CALL>>>
Voda: +255757441463
JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI

No comments:

Post a Comment