YALIYOJIRI KUHUSU SOKA LA ULAYA LEO 13.10.2017 - EDUSPORTSTZ

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Friday, 13 October 2017

YALIYOJIRI KUHUSU SOKA LA ULAYA LEO 13.10.2017


Jose Mourinho
Mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho anataka kumsajili beki wa kushoto wa Tottenham na Uingereza Danny Rose.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 anaweza kuelekea Kaskazini kwa kitita cha pauni milioni 50. (Sun)
Manchester City inatarajiwa kumsajili mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez na inaweza kumnunua mshambuliaji huyo wa Chile kwa kitita cha pauni milioni 20 (Daily Mirror)

Mkufunzi wa zamani wa Everton, Manchester United na Sunderland David Moyes yuko tayari kuanza mazungumzo na Uskochi kuhusu kuwa meneja mpya. (Sun)Watafutaji wa wachezaji katika klabu ya Chelsea watamtazama mchezaji wa Red Star Belgrade's na mshambuliaji wa Ghana Richmond Boakye

Watafutaji wa wachezaji katika klabu ya Chelsea watamtazama mchezaji wa Red Star Belgrade's na mshambuliaji wa Ghana Richmond Boakye, 24, wakati wa mechi ya wiki ijayo ya ligi ya Yuropa dhidi ya Arsenal. (Daily Mail)

Liverpool na Arsenal zote zinamtaka kiungo wa kati wa Monaco na Ufransa Thomas Lemar, 21, msimu ujao. (Daily Mirror)

Manchester City inaweza kumnunua nyota wa Barcelona Messi, lakini mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 30 amekataa kuondoka , kulingana na mchezaji mwenza wa Argentina Sergio Aguero. (TyC Sports, via Talksport)Messi

Messi huenda akaongezewa marupurupu ya hadi £80m iwapo atakubali mkataba mpya na Barcelona. (L'Ara, via Daily Mail)

Chelsea inapanga kumuuza kwa mkopo kiungo wa kati wa Ubelgiji wa timu isiozidi umri wa miaka 21 Charly Musonda, 20, mwezi January. (Evening Standard)

Kiungo wa kati wa Paris St-Germain Grzegorz Krychowiak, 27, anaweza kusajiliwa kwa kandarasi ya kudumu na West Brom (Le10 Sport, via Talksport)

Leicester City inaweza kutaka kumsajili aliyekuwa mchezaji wa Manchester City na Arsenal Bacary Sagna, 34 ambaye atakuwa huru (Leicester Mercury)


like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika Propellerads

For Booking>>>CALL>>>

Voda: +255757441463

JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI
No comments:

Post a Comment