SERGIO AGUERO TAYARI KWA MAPAMBANO MECHI IJAYO - EDUSPORTSTZ

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Friday, 13 October 2017

SERGIO AGUERO TAYARI KWA MAPAMBANO MECHI IJAYOSergio Aguero anahitaji bao moja kufikia rekodi ya ufungaji mabao Manchester City


Sergio Aguero huenda akachezeshwa mechi ya Jumamosi Ligi ya Premia dhidi ya Stoke wiki mbili baada yake kuhusika katika ajali ya barabarani, meneja wa Manchester City Pep Guardiola amesema.

Mshambuliaji huyo wa miaka 29 alitarajiwa kuwa nje kwa wiki kadha baada ya ajali hiyo iliyotokea Amsterdam mnamo 29 Septemba.

Lakini alirejea kwenye mazoezi kamili Alhamisi na meneja wake amesema hali yake ni nzuri.

Alipoulizwa iwapo Aguero atacheza, Guardiola amesema: "Pengine. Hajakuwa sawa 100% lakini amepata nafuu vyema sana."
Aguero arejea mazoezini baada ya ajali

Kiungo wa kati Fabian Delph huenda asicheze kutokana na tatizo misuli ya paja ingawa anafanya mazoezi.

Stoke watakuwa bila ikiungo wa kati Joe Allen aliyeumiwa akichezea Wales.

Mabeki Ryan Shawcross na Bruno Martins Indi pia huenda wasicheze kutokana na majeraha.
 like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika Propellerads

For Booking>>>CALL>>>

Voda: +255757441463

JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI
No comments:

Post a Comment