TAHADHARI KWA MASHABIKI WA SIMBA NA YANGA KATIKA MECHI YA J'MOSI - EDUSPORTSTZ | Habari za Ajira, Mapenzi, Michezo, Elimu, Kilimo, Technology, Siasa na Mziki,

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Tuesday, 24 October 2017

TAHADHARI KWA MASHABIKI WA SIMBA NA YANGA KATIKA MECHI YA J'MOSI

Kuelekea mechi ya watani wa jadi Simba na Yanga, Jumamosi hii, wachezaji waliowahi kuzichezea
klabu hizo, wameelezea namna ambavyo mashabiki wanaweza kuumizwa na matokeo yatakayokinzana na matarajio yao.

Hiyo ni kutokana na timu hizo kushinda kwa idadi sawa ya mabao kabla ya mchezo huo, Simba iliibuka na ushindi mnono dhidi ya Njombe Mji kwa mabao 4-0,huku Yanga wakishinda ugenini dhidi ya Stand United kwa mabao 4-0.

Sekilojo Chambua ni staa wa zamani wa Yanga, alielezea kuwa ; "Hii kila timu kushinda mabao sawa haina maana inaweza kubadili chochote kwenye matokeo zaidi ya kuleta hamasa na mchezo kuwa na presha kubwa, ila ninaloliona ni huku kwa mashabiki ambao wanatambiana kuona kila mtu anaweza kuibuka mshindi, wajiandae kisaikolojia."

Kwa upande wa Bitta John, nyota wa zamani wa Simba, alisema; "Labda kwa Yanga mchezaji tishio naona atakuwa Chirwa, lakini kikubwa makocha wanatakiwa kufanya kazi kubwa ya kuwajenga wachezaji wao kuwa makini wasije wakaingia kwa kuvimba kiasi kwamba wakasahau kazi yao mwisho wa siku wakavuruga mchezo."
like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika Propellerads

For Booking>>>CALL>>>

Voda: +255757441463

JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI
No comments:

Post a Comment