SOMA ALICHOANDIKA HAJI BAADA YA PICHA ZA LISSU KUANZA KUONEKANA - EDUSPORTSTZ

Latest

SOMA ALICHOANDIKA HAJI BAADA YA PICHA ZA LISSU KUANZA KUONEKANA





Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa Timu ya Simba, Haji Manara ambaye ni mwanachama wa CCM amefunguka na kusema hajawahi kumshabiki Tundu Lissu wala CHADEMA lakini anaamini bila uwepo wake na CHADEMA basi chama chake CCM kitalala.


Haji Manara amesema hayo leo baada ya kuona picha ya kwanza ya Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu akiwa hospitali jijini Nairobi nchini Kenya ambapo anapatiwa matibabu kufuatia kupigwa risasi Septemba 7, 2017 na watu wasiojulikana.


"Ohhh God,mimi sijawahi kukushabikia wewe wala chama chako ila nakuombea kwa Mungu upone haraka kaka, urudi katika harakati zako nikiamini bila uwepo wenu chama changu kitalala"aliandika Haji Manara kupitia ukurasa wake wa Instgram.


Mbali na Haji Manara watu wengine wengi wameonyesha kufurahishwa na hali ya Tundu Lissu baada ya kumuona kupitia picha ambazo zimeanza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii, Mbunge huyo wa Singida Mashariki anatarajiwa kupelekwa nje ya nchi kwa matibabu ya awamu ya tatu siku za karibuni.

like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika Propellerads

For Booking>>>



CALL>>>

Voda: +255757441463

JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI










Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz