Mtangazaji aacha kutangaza mechi baada ya kukasirishwa na mechi iliyokuwa ikiendelea - EDUSPORTSTZ

Latest

Mtangazaji aacha kutangaza mechi baada ya kukasirishwa na mechi iliyokuwa ikiendelea



Mtangazaji wa mpira akasirika na kuondoka mechi ikiendelea na kuwawacha watazamaji vinywa wazi

Mtangazaji mmoja wa mpira nchini Urusi alikasirishwa na refa aliyekuwa akisimamia mechi moja na kuondoka katikati ya mechi hiyo na hivyobasi akawaacha watazamaji kuangalia mchezo huo bila maelezo.

Wakati wa mechi hiyo kati ya klabu ya Urusi ya Torpedo Vladmir dhidi ya Tekstilshchik Ivanovo kipa wa Ivanovo alimuangusha mshambuliaji wa upinzani kulingana na kanda za video.

Wakati huo timu hizo mbili zilikuwa 1-1.

Na badala ya kutoa mkwaju wa penalti refa alitoa mkwaju wa adhabu nje ya eneo hatari na kusababisha malalamishi kutoka kwa mashabiki na watazamaji .

Hatua hiyo ilimkasirisha mtangazaji huyo na kuamua kusitisha matangazo aliyokuwa akitoa kulingana na ripoti za Pravda.

Na wakati mkwaju huo wa adhabu ulipopigwa mmoja ya walinzi waliunawa mpira na kuzua madai ya mkwaju mwengine wa penalti lakini refa aliwaambia wachezaji kuendelea na mchezo hatua ilimlazimu mtangazaji huyo kumshutumu vikali refa huyo.Image captionKanda ya video ilionyesha kipa akimwangusha mshambuliaji

Na baada ya shutuma hizo ambapo mtangazaji huyo alimtaja bwana Nikolsky kuwa ''aibu kubwa kwa soka ya Urusi '', aliinuka na kuondoka huku akisema tazameni mechi bila mtangazaji leo .

Mechi hiyo ilikamilika kwa sare ya 1-1.

 like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika Propellerads

For Booking>>>



CALL>>>

Voda: +255757441463

JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI










Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz