MFAHAMU MCHEZAJI BORA WA WIKI VPL - EDUSPORTSTZ | Habari za Ajira, Mapenzi, Michezo, Elimu, Kilimo, Technology, Siasa na Mziki,

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Monday, 16 October 2017

MFAHAMU MCHEZAJI BORA WA WIKI VPL

Ibrahim Ajib amefanikiwa mkuwa mchezaji bora wa wiki baada ya kuwa na kiwango bora dhidi ya Kagera Sugar Jumamosi iliyopita.


Nyota huyo ambaye amejiunga na Yanga msimu huu akitokea klabu ya Simba, ameibuka mchezaji wa wiki kufuatia kuwapiga chini nyota kadhaa waliokuwa na kiwango bora wiki iliyoisha kama Stamili Mbonde, Mkude na wengine

Ajib aliiwezesha klabu yake ya Yanga kuondoka na alama tatu baada ya kutengeneza goli la kwanza lililofungwa na Obrey Chirwa pia na kufunga goli la pili na la ushindi kwa shuti kali la mita 20

Katika mchezo huo ambao Ajib alikuwa moto wa kuotea mbali, alifanikiwa kutengeneza nafasi nyingi za kufunga ambazo hazikutumiwa vizuri na wachezaji wenzake.


Ajibu amefanikiwa kufunga mabao matatu kwenye Ligi Kuu kwa msimu huu.

Baada ya ushindi wa Kagera, Yanga sasa wanakamata nafasi ya tatu baada ya kujikusanyia alama 12 katika michezo 6, pointi sawa na klabu za Simba, Azam, na Mtibwa huku wakitofautiana kwenye magoli ya kufunga na kufungwa.
 like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika Propellerads

For Booking>>>CALL>>>

Voda: +255757441463

JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI
No comments:

Post a Comment