Hatimaye kikosi cha Kagera Sugar kimepata ushindi wa kwanza baada ya kucheza mechi 7 bila ya kushinda hata moja
.
Kagera Sugar imeibuka na ushindi ikiitwanga Ndanda FC kwa mabao 2-1 katika mechi iliyppigwa kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
Ushindi huo utaifanya Kagera Sugar kufikisha pointi sita baada ya kubaki na pointi tatu katika mechi zote 7 kwa kuwa ilipoteza nne na sare tatu.
Wakati Kagera inashima, Singida United imepata sare ya bila kufungana dhidi ya Mtibwa Sugar.
Pia sare nyingine Majimaji imeendelea kwenda mwendo wa kusuasua licha ya kuwa nyumbani baada ya kumaliza kwa 1-1 dhidi ya Mwadui FC.
Lipuli ikiwa nyumbani Iringa, imeripua Mbao FC kwa mabao 2-1 licha ya kwamba wauza mbao hao walitangulia kufunga lakini mchezaji wao wa zamani, Asante Kwassi alisababisha bao la kwanza kabla ya kufunga la pili.
like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika
For Booking>>>
EMAIL: edusportstz@gmail.com
CALL>>>
Voda: +255757441463
JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI
Post a Comment