KESI YA LULU YATIA HURUMA; MAISHA YAKE MIKONONI MWA MAJAJI - EDUSPORTSTZ

Latest

KESI YA LULU YATIA HURUMA; MAISHA YAKE MIKONONI MWA MAJAJI





DAR ES SALAAM: Maskini Lulu! Kesi ya mauaji ya bila kukusudia ya aliyekuwa mwigizaji kinara nchini, Steven Kanumba, inayomkabili staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael Kimemeta almaarufu Lulu, iliyosikilizwa ushahidi wake kwa siku sita mfululizo hadi Alhamisi iliyopita na kuhitimisha saa 144 za kuhenyeshwa mahakamani ambapo kauli za Wazee wa Baraza zimeonekana kuwatisha wengi!
Kesi iliyoweka rekodi kwenye ulimwengu wa mastaa Bongo, ilipangwa kutolewa hukumu yake Novemba 13, mwaka huu katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam.

Mara baada ya kutajwa kwa tarehe hiyo na Wazee wa Baraza kusema Lulu anaingia hatiani kwa kuua bila kukusudia, familia ilipata huzuni na hofu iliyotanda kila kona kwa kuhisi huenda atafungwa bila kujua kwamba mwenye uamuzi wa mwisho ni jaji. Hata hivyo, sheria inasema kwamba, jaji anaweza kumhukumu kifungo cha kwenda jela cha kati ya mwaka mmoja hadi miaka 30 kama ataona ana hatia lakini kama ataona hana hatia, anaweza kumuacha huru.

LIVYOKUWA MAHAKAMANI

Katika kesi hiyo, juzi Alhamisi ilikuwa ni siku ya kuwasikiliza Wazee wa Baraza ambapo jaji anayesikiliza, Sam Rumanyika alikuwa akiwaita wazee hao waungwana. Aliyefungua ukurasa mahakamani hapo alikuwa ni wakili wa upande wa Jamhuri, Faraja George ambaye alimwambia jaji kuwa pande zote mbili zilikuwa tayari kumsikiliza anavyowasomea kesi hiyo Wazee wa Baraza kwa ajili ya kuitolea uamuzi.

Jaji Rumanyika aliwaambia wazee hao kuwa, atawasomea kesi hiyo tangu mashahidi walipoanza kutoa ushahidi wao, nao watatakiwa kutoa uamuzi wao bila kuongozwa na huruma, ahadi, vitisho na vitu vingine kama hivyo. Jaji huyo aliyasoma maelezo yote waliyatoa mashahidi wa pande zote kisha kuwataka kutoa uamuzi.

Wazee hao, kila mmoja kwa wakati wake, walitoa majibu yaliyofanana kuwa Lulu anaingia hatiani kwa mauaji ya bila kukusudia kwa sababu mashahidi wote waliieleza mahakama kuwa, kulikuwa na ugomvi kati ya Kanumba na Lulu kabla ya kifo hicho.

Wazee hao pia walisema kuwa, Lulu ndiye aliyekuwa mtu wa mwisho kuwa na Kanumba kabla ya umauti kumkuta. Kitendo cha wazee hao kutamka hayo, kiliwaduwaza familia ya Lulu na kuonekana kukosa furaha. Baada ya Wazee hao kutoa uamuzi huo, Jaji Rumanyika aliiahirisha kesi hiyo hadi Novemba 13, mwaka huu ambapo ataitolea hukumu.

AWEKA REKODI

Katika kesi hiyo, Lulu aliweka rekodi mbalimbali ikiwemo suala la kujifunika uso kama bibi harusi na kuanza kuwakimbia mapaparazi waliokuwa wakimfuatilia. Rekodi nyingine iliyowekwa kwenye kesi hiyo ni pamoja na kuhudhuriwa na mapaparazi wengi waliokuwa wakiifuatilia kwenye viunga hivyo zaidi ya kesi nyingine zilizokuwa zikiendelea.

Kwa upande wao, Dk Cheni na Baba Lulu walizua maswali kadhaa kwenye kesi hiyo, ambapo wengi walikuwa wakihoji uwepo wa mwigizaji huyo tangu mwanzo hadi mwisho huku akiacha kazi zake. Watu hao walihoji iweje waigizaji wengine waliokuwa karibu na Kanumba kama mshindani wake, Vincent Kigosi ‘Ray’ na wengineo wasionekane kwenye kesi hiyo aonekane peke yake hata kama ndiye aliyemuwekea dhamana.

Wengine walisikika wakihoji kuwa, iweje Baba Lulu naye achukue jukumu la kuwafukuza wanahabari waliokuwa wakimpiga picha mwanaye? Walidai kwani picha hizo zilikuwa na madhara gani kwa mwanaye ambaye ameshapigwa picha nyingi tu mahakamani na wakati mwingine hakuficha uso?

NI MUNGU TU!

Baada ya kutajwa kwa siku hiyo ya hukumu, Novemba 13, baadhi ya wahudhuriaji waliokuwa hawakosi akiwemo Mama Lulu, Lucresia Karugila na mashabiki wa Lulu walisikika wakisema kuwa, kilichobaki sasa ni kumtegemea Mungu tu kwani ndiye hupanga mambo ya kuwapata au kutowapata waja wake.

“Sina cha kusema zaidi ya kumuachia Mungu, ni Mungu tu atakayeamua,” alisikika mama Lulu akigoma kuzungumza na vyombo vya habari. Lulu anayetetewa na Wakili Peter Kibatala, anakabiliwa na kesi ya kumuua bila kukusudia mwigizaji Kanumba aliyekuwa mwandani wake, kosa analodaiwa kulitenda Aprili 7, 2012, nyumbani kwa staa huyo, Sinza-Vatican jijini Dar

like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika Propellerads

For Booking>>>



CALL>>>

Voda: +255757441463

JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI










Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz