KAMA ULIFATILIA MECHI ZA JUMAMOSI 14/10/017 EPL UTAKUBALIANA NA HAYA - EDUSPORTSTZ

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Sunday, 15 October 2017

KAMA ULIFATILIA MECHI ZA JUMAMOSI 14/10/017 EPL UTAKUBALIANA NA HAYA


1.United wanazuilika kabisa, ilikuwa suluhu 3 ambayo haikuwa na mabao kati ya Liverpool na Manchester United, lakini mchezo wa leo Anfield umeonesha United wanaweza kuzuilika kabisa huku walinzi wa Liverpool wakimpoteza nyota wao Romelu Lukaku,ni wazi United kama sio De Gea wangekufa.
Katika suluhu hiyo mlinzi wa kulia wa Manchester United Antonio Valencia aliweka rekodi kuwa mchezaji wa kwanza ambaye sio mzaliwa wa bara la Ulaya kuichezea United michezo 300.Chelsea

2.Chelsea kama popo, Goli la kuongoza la Crystal Palace liliwafanya Palace kukomesha njaa yao ya ufungaji ambayo imedumu kwa muda wa masaa 12 na hilo lilikuwa bao lao la kwanza kupata katika mashuti 86 waliyopiga msimu huu.
Chelsea msimu huu imekuwa  haieleweki kwani kuna wakati wanaonekana wamechoka sana lakini kuna wakati wanaonekana kujaribu kurudi, kipigo cha leo kimewarudisha nyuma kwani wangeshinda wangepunguza pengo la alama na timu zilizoko juu yao.
3.Pep anataka kombe tu sio hadithi, Etihad panaonekana sasa sio mahalinpakwenda kabisa, wapinzani, timu mbili kabla ya Stoke zilizofika Etihad zilikufa bao 5 huku leo Stoke City akila 7 kwa 2 ambazo kwa mahesabu mengine ni sawa na 5 bila, usajili aliofanya na matokeo anayopata vinaonesha wazi anataka ndoo.
4.Wenger arudi kwenye sack race, Arsenal Wenger ameanzishiwa tena mabango ya Wenger Out ambayo yalishaanza kupotea, kipigo cha bao 2 kutoka kwa Watford kimeamsha hisia kali kwa mashabiki wa klabu hiyo na wameshaanza kutuma  ujumbe wa Wenger out mitandaoni na sasa anarejea katika mbio za kufukuzwa.
5.Wembley sio parahisi kwa Tottenham, mashabiki wa Tottenham hawapapendi Wembley na wengi wanaamini wana mkosi na uwanja huo, leo wamepata ushindi wao wa kwanza katika uwanja huo.
Lakini kwa Tottenham ya sasa ilikuwa wazi kwamba kucheza na timu ya chini kama Afc Bournemouth kulitarajiwa mabao mengi lakini wamepata ushindi mwembamba sana wa bao mja dhidi ya Bournemouth.

 like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika Propellerads

For Booking>>>CALL>>>

Voda: +255757441463

JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI
No comments:

Post a Comment