ARJEN ROBBEN ASTAAFU SOKA LA KIMATAIFA - EDUSPORTSTZ

Latest

ARJEN ROBBEN ASTAAFU SOKA LA KIMATAIFA



MKONGWE wa Uholanzi, Arjen Robben ametangaza kustaafu soka ya kimataifa usiku wa jana baada ya kuifungia mabao mawili timu yake dhidi ya Sweden katika mchezo wa Kundi A kufuzu Kombe la Dunia.

Robben alifunga mabao yote jana Uholanzi ikishinda, lakini ikashindwa kufuzu fainali za Kombe la Dunia mwakani, baada ya kuzidiwa wastani wa mabao na Sweden kufuatia kulingana kwa pointi 19.

Winga huyo machachari alikaribia kudondosha machozi jana kabla na baada ya mechi Uwanja wa Amsterdam Arena.

"Ni wakati mzuri kukabidhi mwenge kwa kizazi kijacho,"alisema.

Alisema kwamba Uholanzi imeshindwa kufuzu Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2002. "Tulijua kabla ya mchezo huu, itakuwa vigumu kwetu kwenda Kombe la Dunia,".

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33, katika kipindi chake cha miaka 14 ya kuichezea timu yake ya taifa, amekuwa mwenye mafanikio, akifunga jumla ya mabao 37 na kutoa pasi za mabao 29 katika mechi 96.

Alikuwa tegemeo la Uholanzi ikishika nafasi ya pili katika Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2010 kabla ya kumaliza nafasi ya tatu nchini Brazil miaka mitatu iliyopita.

Atakumbukwa pia kukosa bao la wazi mno dhidi ya Hispania kwenye fainali Afrika Kusini.

Kipa Iker Casillas alifanya kazi nzuri mno kuokoa mchomo wa Robben kabla ya Hispania ikienda kushinda 1-0 katika dakika za nyongeza.

"Ilikuwa safari ndefu, miaka 14," alisema. "Kumbukumbu yangu ya kwanza pia ilikuwa dhidi ya Sweden mwaka 2004 wakati nilipokuwa mdogo mno. Nilipiga penalti ya ushindi tena mwaka 2004, mashindano yangu ya kwanza,".

"Nimecheza michuano sita, Euro tatu na Kombe la Dunia tatu na matokeo mazuri yalikuwa mwaka 2010 na 2014.

"Tulikuwa nchi ndogo na mara moja tulikuwa wa pili na mara moja wa tatu. Tunaweza kujivunia mno hili,"alisema.like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika Propellerads

For Booking>>>



CALL>>>

Voda: +255757441463

JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI










Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz