REKODI ZITAKAZOWEZA KUMFANYA CHRISTIAN RONALDO KUWA MCHEZAJI WA KARNE - EDUSPORTSTZ

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Wednesday, 27 September 2017

REKODI ZITAKAZOWEZA KUMFANYA CHRISTIAN RONALDO KUWA MCHEZAJI WA KARNE

REKODI ZA CHRISTIAN RONALDOKatika mara 7 ambazo Real Madrid wameenda kukipiga Ujerumani jana ilikuwa mara yao ya kwanza kupata ushind, Cristiano Ronaldo alifunga mara mbili huku Gareth Bale akifunga lingine katika ushindi wa mabao 3 kwa 1.

Mengi yameongelewa lakini takwimu zinaonesha Ronnaldo amekuwa striker ambaye hashikiki haswa linapokuja suala la champions league na namba zinaonekana wazi jinsi Mreno huyu alivyo na urafiki na nyavu.

Katika michezo 400 ambayo Ronaldo ameichezea Real Madrid mshambuliaji huyu amewapa Madrid mabao 4111 huku kati ya hayo akifunga hat trick 42.

Cristiano Ronaldo ameshapiga assist 112 huku akiweka kabatini jumla ya makombe 13 toka ajiunge na Real Madrid, rekodi inayoonesha wazi jinsi gani pamoja na miaka yake 31 lakini ni mpiga kazi haswa.

Katila Champions League huko ndiko hakamatiki kabisa kwani idadi ya mabao aliyofunga ni kubwa kuliko michezo aliyocheza, ameweka kambani mara 93 hiyo ikiwa pungufu ya michezo mitatu aliyocheza(amecheza 90).

Kingine ambacho kinatisha zaidi ni kwamba Ronaldo amehusika katika mabao 513 ya Real Madrid waliyofunga, huki akifunga mara 14 katika michezo 9 waliyocheza Champions League mwaka huu.

Lakini je unajua kwamba mashuti 6 kati ya 7 ya mwisho ambayo Ronaldo aliyapiga langoni mwa wapinzani katika Champions League yalikwenda moja kwa moja nyavuni na ni moja tu ambalo lilizuiliwa.
 like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika Propellerads

For Booking>>>CALL>>>

Voda: +255757441463

JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI
No comments:

Post a Comment