MAKOSA YA KAMUSOKO KUIGHALIMU YANGA NA KUMPA MZIGO TSHISHIMBI - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

Tuesday, 26 September 2017

MAKOSA YA KAMUSOKO KUIGHALIMU YANGA NA KUMPA MZIGO TSHISHIMBI

MASHABIKI wa Yanga hawafurahishwi na ushindi mwembamba inaoupata timu yao na taarifa hizo zimemfikia kocha wao, George Lwandamina naya akanena mengi juu ya sakata hili.

Kocha huyo ameshangazwa na wasiwasi wa mashabiki, lakini akakiri kama si Kabamba Tshishimbi kuwa fiti ingekuwa mtihani mkubwa. Hata hivyo kasema anajua cha kufanya.

Lwandamina alisema Yanga yake bado haijafanya vibaya kama wengi wanavyopaza sauti na kwamba ukiondoa Simba ambayo ilipata ushindi mkubwa katika mchezo mmoja, hakuna timu nyingine iliyokuwa na mfululizo wa kupata mabao mengi.

“Nimesikia kuna ambao hawafurahishwi na timu kushinda bao moja, lakini kwangu naliona katika mtazamo tofauti, sidhani kama Yanga imefanya vibaya kama wanavyosema,” alisema Mzambia huyo.

“Ukiangalia hakuna timu inayokuwa inashinda mabao mengi ambayo ungesema sisi hatuko sawa, timu nyingi zimekuwa zikipata ushindi mwembamba ukiondoa Simba ambao walipata ushindi mkubwa katika mchezo mmoja tu.

“Najua watu wanataka mabao mengi hata sisi kama makocha hiyo ni kiu yetu, lakini mambo lazima yafanyike kiufundi. Ukiangalia mechi zetu nne tulizocheza, utagundua mchezo wetu wa mwisho ndiyo tumetengeneza nafasi nyingi, lakini shida ikaja vijana walishindwa kuzitumia hilo ndiyo jukumu letu sasa.”

Lwandamina ambaye ni mara chache huzungumza na vyombo vya habari kutokana na mara nyingi kumuachia kazi hiyo msaidizi wake, Shadrack Nsajigwa, aliongeza: “Kuna wachezaji wetu baadhi wameshindwa kuwa katika ubora wao, mfano Kamusoko ni mtu muhimu kwetu, lakini ukiangalia bado sijaridhika na uwezo wake, naamini anaweza kufanya vizuri zaidi, kama mtakumbuka usajili wake ulichelewa kidogo hatua hiyo ikamfanya akose maandalizi ya awali ya msimu kwa asilimia kubwa.

“Alikuja tukiwa Morogoro, lakini kukosa programu hiyo kunamfanya sasa kuyumba kidogo.

“Kwa sasa tumekuwa tukinufaika zaidi kwa ufanisi wa Papii (Tshishimbi) ambaye alikuja akiwa vizuri lakini endapo hatutalifanyia kazi hili la Kamusoko kwa haraka, tunaweza kumfanya Papii naye akapungua ubora kutokana na atakuwa akifanya kazi kubwa zaidi peke yake.


“Hatujakata tamaa, tunaona sasa anazidi kupambana kuna kazi tulishaianza kwake na sio yeye tu hata Ngoma (Donald) naye alikosa sehemu fulani ya maandalizi yale, naye taratibu ameanza kurudi.

“Tulipaswa kuanza kuandaa timu kwa kuwa na wachezaji wote kwa pamoja, lakini hatukuweza kulifanikisha hilo kutokana na majukumu ya kumalizia usajili, kama uongozi ulifanya majukumu yake katika mazingira ambayo binafsi naelewa ugumu ulivyokuwa.

“Tambwe (Amissi) ameanza kurudi, nafikiri kama atafanikiwa kuwa katika ubora wake. Kuna ushindani utaongezeka zaidi kwa washambuliaji wenzake, hapo tunaweza kufanya maboresho zaidi kwa kuongeza ufanisi wa washambuliaji kwa kuweza hata kumpeleka Chirwa (Obrey) atokee kulia.”

Kocha huyo anaamini msimu huu ligi ni ngumu na mashabiki wanapaswa kuiangalia kwa mtazamo mpana.

Baada ya mapumziko ya siku moja, Lwandamina alikirudisha kikosi chake kuanza maandalizi ya kuikaribisha Mtibwa Sugar akiwarudisha vijana wake gym walikofanya mazoezi kwa siku ya jana Jumatatu asubuhi.like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika Propellerads

For Booking>>>CALL>>>

Voda: +255757441463

JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI