MOURINHO AWATEMEA CHECHE ZA KEJERI CHELSEA - EDUSPORTSTZ | Habari za Ajira, Mapenzi, Michezo, Elimu, Kilimo, Technology, Siasa na Mziki,

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Monday, 18 September 2017

MOURINHO AWATEMEA CHECHE ZA KEJERI CHELSEA


Mourinho alisema uwezo wa Manchester United kuwa na pesa za kutosha na kuzitumia, ndio uliowafanya wawashinde Chelsea kwa mbio za kumsajili Lukaku kutoka Everton.

Manchester, England.Kocha Jose Mourinho ameipiga dongo klabu ya Chelsea kwa kusema kilichowashinda kwenye mpango wao wa kumsajili, Romelu Lukaku. Hawana pesa.

Mourinho alisema uwezo wa Manchester United kuwa na pesa za kutosha na kuzitumia, ndio uliowafanya wawashinde Chelsea kwa mbio za kumsajili Lukaku kutoka Everton.

Mourinho alisema: “Wala sio ushawishi wangu. Nadhani ni kwa sababu tulitoa pesa ambayo Everton waliitaka na tumempa mshahara ambao mchezaji mwenyewe aliutaka na kulipa ada ya mawakala, ni hivyo tu hakuna sababu nyingine.”

Lukaku alikuwa mteja mwingine wa wakala Mino Raiola kutua Man United ya Jose Mourinho baada ya awali kuwapeleka Paul Pogba, Zlatan Ibrahimovic na Henrikh Mkhitaryan.

like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika
Edusportstz

For Booking>>>CALL>>>

Voda: +255757441463

JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI
No comments:

Post a Comment