BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Monday, 4 September 2017

MANCITY KATIKA TASWIRA MPYA YA UEFA


Shirikisho la soka nchini Hispania La Liga liliandikia barua shirikisho la soka barani Ulaya UEFA wakitoa malalamiko kuhusu ukiukwaji wa sheria za matumizi FFP unaofanywa na klabu ya Man City.

Raisi wa La Liga Javier Tebas alitoa malalamimo kuhusu wamiliki wa klabu ya Manchester City ambao pia na wamiliki wa klabu ya PSG kutokana na matumizi makubwa ya kifedha wanayoyafanya.

Lakini baadaye shirikisho la soka la UEFA lilitoa majibu kuhusiana na barua iliyoandikwa na raisi wa La Liga kwa kusema kwamba shirikisho hilo halitaichunguza klabu hiyo na taarifa nyingine kinyume na hapo ni uongo.

Taarifa hiyo imesema “Uefa hatutaichunguza Manchester City kuhusiana na sheria za matumizi (FFP) na kama kuna taarifa nyingine tofauti na hiyo itakuwa sio ya kweli” ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

La Liga walituma barua hiyo siku ya leo kuhusiana na kuzichunguza PSG na pia Manchester City kutokana na vilabu hivyo kutumia pesa nyingi sana katika dirisha moja la usajili.

Psg na Manchester City wote wanamilikiwa na matajiri wa Qatar na toka wamezichukua timu hizo zimekuwa na matumizi makubwa sana ya pesa hali ambayo raisi wa La Liga amesema ni tishio kwa soka.

No comments:

Post a Comment