KIM POULSEN KUWEKA KAMBINI KIKOSI CHA WACHEZAJI 50 NGORONGORO HEROS - EDUSPORTSTZ | Habari za Ajira, Mapenzi, Michezo, Elimu, Kilimo, Technology, Siasa na Mziki,

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Friday, 29 September 2017

KIM POULSEN KUWEKA KAMBINI KIKOSI CHA WACHEZAJI 50 NGORONGORO HEROS

 KOCHA NGORONGORO HEROS

Kocha mkuu wa timu za taifa za vijana, Kim Poulsen amewaita wachezaji 50 kwa ajili ya kambi ya wiki mbili kujiandaa na mashindano ya kuwania kufuzu fainali za Afrika kwa vijana mwaka 2019 zitakazofanyika Niger.

Poulsen amesema kati ya wachezaji hao, 23 ni wale waliokuwemo kwenye kikosi cha timu ya taifa ya vijana ya Serengeti Boys kilichoshiriki fainali za Afrika mwaka huu zilizofanyika Gabon.

"Wachezaji wote walioitwa ni wale waliozaliwa kuanzia mwaka 1999, ambapo baada ya kambi hiyo ya wiki mbili, watachujwa na kubakia 30 ambao tutakuwa tukifanya mazoezi ya mara kwa mara ili kujiandaa na kibarua kilicho mbele yetu," alisema Poulsen.

Katika nyota hao walioitwa, miongoni mwao yupo mshambuliaji wa Mtibwa Sugar, Riffat Khamis ambaye hakuwemo katika kikosi cha Serengeti Boys.
like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika Propellerads

For Booking>>>CALL>>>

Voda: +255757441463

JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI
No comments:

Post a Comment