USIYOYAJUA KUHUSU SOKA LA ULAYA SIKU YA LEO TAR 28 AUGUST 2017 - EDUSPORTSTZ

Latest

USIYOYAJUA KUHUSU SOKA LA ULAYA SIKU YA LEO TAR 28 AUGUST 2017



Swansea watapanda dau la pauni milioni 13 kutaka kumsajili tena mshambuliaji wa Manchester City Wilfried Bony, aliouzwa kwenda City kutoka Swansea mwaka 2015 kwa pauni milioni 28. (Daily Mail)

Inter Milan wanakaribia kumsajili Keita Balde wa Lazio kwa pauni milioni 27. (Daily Mirror)

Birmingham City wanazungumza na kiungo wa kimataifa wa Ghana Afiriye Acquah, 25, kutaka kumsajili kutoka Torino. (Sky Sports

Liverpool wamemuulizia kiungo wa Monaco Thomas Lemar, 21, na wapo tayari kuvunja rekodi ya uhamisho ya klabu kwa kutoa pauni milioni 55. (Daily Telegraph)

Paris Saint-Germain wamefikia makubaliano ya kumsajili kwa mkopo kwanza, mshambuliaji wa Monaco, Kylian Mbappe, 18, na kuweza kukamilisha usajili wa pauni milioni 166 msimu ujao. (L'Equipe)

Manchester United wamewapa Real Madrid pauni milioni 92 kutaka kumsajili Gareth Bale. (Daily Star)

Barcelona wanamuona Marcus Rashford wa Manchester United kama mrithi wa baadaye wa Luis Suarez. (Don Balon)

Chelsea wana uhakika wa kukamilisha uhamisho wa pauni milioni 30 wa kiungo wa Leicester City Danny Drinkwater, 27, kabla ya dirisha la usajili kufungwa. (Daily Telegraph)

Manchester City wapo tayari kuwapa Arsenal pauni milioni 70 pamoja na beki Jason Denayer, ili kumsajili Alexis Sanchez, 28. (Daily Star)

Manchester City wanajiandaa kupanda dau kumtaka mshambuliaji wa Borussia Dortmund Pierre Emerick Aubameyang, iwapo watashindwa kumsajili Alexis Sanchez. (Le10Sport)Marcus Rashford na Zlatan Ibrahimovic

Leicester City wamepanda dau la pauni milioni 23 kutaka kumsajili beki wa West Brom Jonny Evans, 29. (BBC)

Hatma ya meneja wa Crystal Palace iko mashakani baada ya kupoteza mechi tatu za EPL. (Guardian)

Meneja wa West Ham Slaven Bilic anapambana vikali kulinda kazi yake baada ya kupoteza mechi tatu za mwanzo za EPL. (Sun)

Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp amesema yuko tayari kumruhusu Divock Origi, 22, kuondoka kwa mkopo iwapo klabu yake itaongeza wachezaji wapya kabla ya dirisha la usajili kufungwa. (Liverpool Echo)

Beki wa Arsenal Shkodran Mustafi, 25, anajiandaa kuondoka Emirates na kwenda Inter Milan, mwaka mmoja tu baada ya kusajiliwa kwa pauni milioni 35 kutoka Valencia. (ESPN)Shkodran Mustafi

Stoke City wamefikia makubaliano na Tottenham ya kumsajili beki Kevin Wimmer, 24, kwa pauni milioni 15. (Sky Sports)

Mshambuliaji wa Chelsea Loic Remy, 30, ananyatiwa na Las Palmas ya Uhispania na Calgiari ya Italia. (Daily Mail)

Meneja wa Chelsea atabakia Stamford Bridge hata kama watashindwa kuongeza wachezaji wengine wapya. (Evening Standard)

Chelsea wanataka kumsajili mshambuliaji wa Swansea Fernando Llorente, 32, wakilenga kusajili wachezaji watatu wapya kabla ya dirisha la usajili kufungwa. (Independent)

Kipa wa Liverpool Simon Mignolet, 29, ananyatiwa na Napoli. (Gianluca Di Marzio)

West Brom wamepanda dau la pauni milioni 10 kumtaka kiungo wa Fenerbahce Josef de Souza, 28, na pia wamemuulizia beki wa Bournemouth Tyrone Mings, 24. (Daily Mail))


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz