BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Monday, 28 August 2017

MSUVA AZIDI KUWEKA REKODI YAKE SAFI LIGI YA MOROCCOWinga wa kimataifa wa Tanzania, Simon Happygod Msuva, jana ameisaidia timu yake, Difaa Hassan El-Jadida kufuzu kwenye Raundi ya Pili ya michuano ya Kombe la Ligi Morocco, maarufu kama Throne Cup baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya CR Khemis Zemamra Uwanja wa Grand Prix mjini Marrakech.

Msuva aliyejiunga na Difaa Hassan El-Jadida mwezi uliopita kutoka kwa mabingwa wa Tanzania, Yanga SC jana alifunga bao la tatu dakika ya 62 katika mechi yake ya kwanza rasmi ya mashindano.

Hiyo ni baada ya beki Marwan Aghudy kufunga bao la kwanza dakika ya 28 na mshambuliaji Bilal Almkra kufunga la pili dakika ya 34.

No comments:

Post a Comment