MPYA; TAZAMA SAKATA LA USAJILI NA SOKA KWA SIKU YA LEO - EDUSPORTSTZ

Latest

MPYA; TAZAMA SAKATA LA USAJILI NA SOKA KWA SIKU YA LEO

Costa alifunga mabao 20 katika mechi 35 alizochezea Chelsea na kuwasaidia kushinda ligi msimu uliopita

Chelsea wanajiandaa kumuuza Diego Costa kwa hasara. (Sun)

Ivan Perisic alifunga mabao 18 Serie A misimu miwili aliyokaa Italia

Manchester United wanataka kumsajili kiungo wa Monaco Thomas Lemar. (Daily Record)

Manchester United bado wana matumaini ya kukamilisha usajili wa Ivan Perisic. (Mirror)

Tottenham wamefikia makubaliano ya kimsingi ya kumsajili Davinson Sanchez, 21, kutoka Ajax kwa pauni milioni 28 na milioni 14 zaidi kama marupurupu. (Independent)

Manchester City wapo tayari kuwapa West Brom pauni milioni 22 ili kumsajili nahodha wao Jonny Evans, 29, baada ya dau la pauni milioni 18 kukataliwa, na watampa mara mbili ya mshahara wa pauni 75,000 kwa wiki anaolipwa sasa. (Mirror)

Dau la Chelsea la pauni milioni 62 kumtaka beki wa Juventus Alex Sandro, limekataliwa. (Mirror)

Mkurugenzi wa michezo wa Barcelona Robert Fernandez amesema itakuwa "vigumu" kumsajili kiungo wa Liverpool Philippe Coutinho, 25, kwa sababu hana kipengele cha uhamisho kwenye mkataba wake. (Liverpool Echo)

Barcelona "watapigana" mpaka siku ya mwisho ya usajili ili kumsajili Philippe Coutinho kutoka Liverpool. (Telegraph)

Mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa, 28, amesema hatorudi Stamford Bridge na anataka kujiunga na Atletico Madrid. (Telegraph)

Everton huenda wakamtaka Diego Costa kwa mkopo. (Sun)

Beki wa Tottenham Kevin Wimmer, 24, anazungumza na Stoke City kuhusu uhamisho wake wa pauni milioni 15. (Telegraph)

Stoke City pia wanataka kumsajili Kevin Wimmer kutoka Spurs. (Stoke Sentinel)

Beki wa Arsenal Gabriel, 26, anakaribia kujiunga na Valencia kwa pauni milioni 10. (Evening Standard)Fabinho

Paris Saint-Germain bado wanataka kumsajili kiungo mkabaji wa Monaco, Fabinho, 23. (L'Equipe)

Kiungo wa PSG Blaise Matuidi, 30, amekamilisha vipimo vya afya Juventus, lakini timu hizo mbili bado hazijakubaliana jinsi ada ya uhamisho itakavyolipwa, huku meneja wa PSG Unai Emery akisema hakutaka kumuuza mchezaji huyo. (Le Parisien)

Wakurugenzi wa Borussia Dortmund wamesema Barcelona "hata hawapo karibu" katika kufikia dau la mshambuliaji wake Ousmane Dembele, 20. (Kicker)Gabriel

Fiorentina wamemwambia mshambuliaji wake Nikola Kalinic, 29, anayenyatiwa na AC Milan kuwa atapigwa faini kwa kutotokea mazoezini siku ya Alhamisi. (Sun)
.


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz